Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
DIWANI wa Kata ya Bonyokwa, TUMIKE MALILO amezindua Bonanza la Kata ya BONYOKWA kwa kushirikisha timu za kata hiyo kuamasisha wananchi na vijana wajisajili katika kadi za mfumo wa ELECTONIC na Daftari la mpiga kura.
Katika Bonanza hilo Diwani Tumike Malilo alishirikisha timu nane kutoka katika mitaa minne ya Kata ya Bonyokwa kila mtaa timu mbili ziliweza kushiriki.
“Katika kata yangu ya Bonyokwa leo tumezindua Bonanza la Tumike Malilo dhumuni la Bonanza hili ni kuhamasisha wananchi wa Bonyokwa kujisajili katika kadi za kisasa za Electronic za Chama cha Mapinduzi CCM pia kutoa elimu ya Ulinzi shirikishi kwa jamii waweze kulinda na kulipa ada na KUJIANDIKISHA katika Daftari la mpiga kura waweze kupata haki ya msingi ya kupiga kura “alisema “alisema Tumike .
Aidha Diwani Tumike aliwataka wananchi wa Bonyokwa kujisajili katika Daftari la mpiga kura kwenye mfumo wa ELECTONIC na kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Pia katika Bonanza hilo walishirikisha timu za Rede za Bonyokwa,Kimanga na Kisukuru kwa ajili ya kujenga mahusiano na Umoja wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Alisema Bonanza hilo litakuwa endelevu kwa timu za Bonyokwa kwa ajili ya kuhamashisha viwanja washiriki katika Daftari la mpiga kura waweze kupata haki yao ya Msingi waweze kumpigia kura Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa Rais wabunge na madiwani mwaka 2025.
Katika hatua nyingine Diwani Tumike aliloa elimu kwa wananchi wake akiwataka wakifika Polisi wasimamie Sheria na kufuata haki huduma za jeshi la Polisi kituo cha Polisi chochote zinatolewa bure bila pesa .
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Ukonga ,ASP Novatus Mallya ,alisema Suala la Ulinzi Shirikishi sio SIASA lipo kisheria wananchi wanatakiwa kulipa ada na kulinda Polisi usiku katika maeneo yao kwa ajili ya kuimarisha usalama wa wananchi kudhibiti waharifu kabla Jeshi la Polisi kufika.
Mkuu wa Polisi Jamii Wilaya ya Ukonga Novatus alisema wanatoa Elimu ya Ulinzi shirikishi wananchi waweze kulinda inapotokea uharifu vikundi vya ulinzi wanadhibiti waharifu katika maeneo yao.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025