Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), lipo mkoani Kagera kwa ajili ya kutoa elimu ya Uhifadhi na Utalii hasa katika vijiji zilivyopakana na hifadhi mkoani humo.
Timu ya TANAPA ipo Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, kutoa elimu katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi, mashuleni pamoja na kutembelea wadau wa Utalii Kanda ya Ziwa hususani mji wa Bukoba.
Lengo la kufanya hivyo ni kuhamasisha wananchi kutembelea vivutio vya utalii na kuchangamkia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Hifadhi za Taifa zilizopo mkoani Kagera Ibanda – Kyerwa na Rumanyika Karagwe.
Akizungumza akiwa Wilayani Bukoba, Afisa Uhifadhi Mkuu na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano TANAPA, Catherine Mbena amesema wapo Wilayani humo kwa ajili ya kuubarisha Umma juu ya shughuri za Uhifadhi na Utalii zinazofanywa na Shirika hilo.
“Mji wa Bukoba umekuwa njia rahisi kwenda kweye maeneo mengi ya Hifadhi za Taifa, hapa ndipo ndege zinatua lakini meli pia huwa zinatia nanga pamoja na magari mengi kupita katika wilaya hii.
“Kwetu TANAPA unaelekea hifadhi ya Taifa ya Ibanda-Kyerwa, Rumanyika-Karagwe, Burigi-Chato pamoja na visiwa vya Rubondo. Kutoka hapa kwenda Ibanda-Kyerwa Kilometa 221, kuelekea Rumanyika-Karagwe Kilometa 171.
“Tumekuja hapa kuendelea kutoa elimu na tutaingia katika hifadhi ya Taifa ya Ibanda-Kyerwa na baadae tutakwenda hifadhi ya Taifa ya Rumanyika-Karagwe ili kukuhabarisha Mtanzania kuhusu shughuri za Uhifadhi.
“Lakini pia kukuhamasisha kuhusu kutembelea vivutio vilivyopo katika maeneo haya ya hifadhi za Taifa Tanzania,” amesema PCO Catherine.
Hata hivyo amewataka Watanzania wote waliopo Kanda ya Ziwa, kupigia kura Mlima Kilimanjaro na Hifadhi ya Taifa Serengeti katika kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za World travel awards 2024.
“Usisahau kupigia kura Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hifadhi bora Barani Afrika, na hii itakuwa mara ya sita mfulululizo ninaamini tutashinda, pia upigie kura Mlima Kilimanjaro kuwa kivutio bora barani Afrika na ushashinda mara tatu, hii itakuwa mara ya nne,” amesema.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa