Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WIZARA ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum imesema katika kutekeleza viaumbele vyake sita imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2024/25 ya Shilingi 67,905,259,000.
Akiwasilisha Makadirio ya bajeti hiyo jijini hapa,leo Mei 17,2024,Bungeni Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Dorothy Gwajima
amesema kuwa kati ya fedha hizo, Shilingi 47,487,079,000 ni fedha za matumizi ya kawaida ambapo Shilingi 21,650,426,000 ni Fedha za Mishahara na Shillingi 25,836,653,000 ni fedha za uendeshaji wa ofisi.
“Aidha, Shilingi 20,418,180,000 ni fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo Shillingi 18,025,673,000 ni fedha za ndani na Shillingi 2,392.507,000 ni fedha za nje,” amesema.
Pia Waziri Gwajima ametaja baadhi ya maeneo yaliyotengewa fedha kwa mwaka 2024/25 kuwa ni pamoja na Katika eneo la kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi (Generation Equality Forum – GEF), kiasi cha shilingi bilioni 3.2 zimetengwa.
Waziri Dkt.Gwajima ametaja vipaumbele hivyo sita kwa mwaka 2024/25 kuwa ni kukuza ari ya jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa
Kuratibu afua za kukuza usawa wa kijinsia na kutokomeza vitendo vya ukatili, uwezeshaji wanawake kiuchumi, upatikanaji wa haki, ulinzi na malezi chanya ya watoto Kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za msingi za ustawi wa jamii.
Kutambua, kuratibu na kuendeleza Makundi Maalum wakiwemo wafanyabiashara
ndogondogo.
Kuboresha mazingira ya kufundisha na
kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na Kuimarisha ushiriki na mchango wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa