November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Dkt. Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Oxford Policy Management

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dodoma

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy Management kuhusu Uwezekano wa matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence and Machine Learning) katika kufanya mapitio ya matumizi ya umma (Public Expenditure Review).

Kikao hicho kimefanyika tarehe 09 Mei 2024 ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi amesema pia lengo la kikao hicho ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD) nchini Tanzania.

Ikumbukwe Serikali ya Tanzania ilizindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali yam Mtoto (PJT-MMMAM) mwaka 2021 kama mpango mkuu wa kuzileta pamoja Wizara na wadau mbalimbali ili kuboresha Makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 8.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Wataalam kutoka Oxford Policy Management Ofisini kwake tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Adela Mpina (Kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Wataalam kutoka Oxford Policy Management, Kushoto ni Mkururgenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma.
Mshauri Elekezi kutoka Oxford Policy Management (OPM) Dkt. Emmanuel Maliti akieleza jambo katika kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea Ofisini kwake tarehe 09 Mei , 2024 Jijini Dodoma.