November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kajigila atoa tuzo kwa walimu Bagamoyo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

AFISA Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya BAGAMOYO, Wema Kajigili ametoa tuzo kwa Walimu Wakuu wa shule za Msingi za Serikali na Binafsi wilayani BAGAMOYO kwa kuongeza ufaulu idara ya Elimu msingi kufanya vizuri Kitaifa.

Akitoa tuzo hizo Afisa Elimu Kajigili, alisema ni sehemu ya utaratibu wake endelevu katika kuwapa moyo walimu kutokana na jitihada zao kubwa wanazofanya katika wilaya ya Bagamoyo katika kukuza sekta ya elimu msingi mpaka kufikia kufanya vizuri kitaaluma.

“Leo ni siku ya utoaji Tuzo katika shule zilizofanywa vizuri zilizofanya vizuri katika mitihani ya Taifa kwa darasa la saba na mitihani ya upimaji darasa la nne mwaka 2023 ambapo katika wilaya yangu tulipata asilimia 93.8 kati ya asilimia 85 za ufaulu Kitaifa kwa PSLE na mtihani wa UPIMAJI darasa la nne Halmashauri ilipata asilimia 99.9” alisema Kajigili

Aidha Afisa Elimu Mwalimu Kajigili alisema Halmashauri hiyo ilishika nafasi katika stadi za kusoma ,kuhesabu na Kuandika (KKK )Kitaifa Bagamoyo idara ya Elimu Msingi imeshika nafasi ya tatu Kitaifa, katika utoaji chakula shuleni Lishe kwa wanafunzi.

Pia alisema Bagamoyo idara ya elimu msingi imeshika nafasi ya tatu Kitaifa katika ufatiliaji yaani KPI (Key Prefomance Indicator ) zote hizo ni juhudi za ushirikiano wa Walimu wake,Waratibu Elimu kata, wadhibiti ubora wameipaisha sekta ya elimu Bagamoyo.

Baadhi ya shule zilizopata tuzo hizo Kaole,Ukuni,Nia Njema,Majengo,Mbegani,Zinga,Buma,Mbaruku,Kiromo,Pande,Miembe saba Mkenge,Bigilo, Mwanamakuka,Royal,Victoria na shule Binafsi, Royal Premer ,Daniel ,Boumjuo.

Wakati huo huo alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan , kwa kufanya mambo makubwa sekta ya Elimu msingi kuwekeza kwa ajili ya elimu ambapo Serikali imeweza kujenga vyumba vya madarasa 132 kwa kushirikiana na wadau wa elimu .

Pia alisema wamepokea kompyuta 60 kutoka kwa wadau wa sekta ya Elimu pamoja na nyumba nane za Walimu zimejengwa na Serikali pamoja na matundu ya vyoo 357 na ongezeko la shule saba mpya za msingi.
Kwa kipindi cha miaka mitatu.

“Serikali inaendelea kujenga shule zingine saba ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani shule hizi saba zinajengwa kata ya Kerege eneo la kilemela ,Kata ya Nia njema eneo la Kimarang ‘ombe kata ya magomeni Sanjale,Kata ya Fukayosi,Kalimeni,kata ya Zinga Gogoni, kata ya Yombo ,Kiegei na Kwedibaha

Kwa upande wake Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule Halmashauri ya Bagamoyo Neema Muhondwa, alitoa tuzo kwa Maafisa Elimu kata kwa kufanya vizuri kitaaluma mpaka Halmashauri hiyo kungara Kitaifa ambapo aliwataka Waratibu Elimu kata waendelee kushirikiana na Serikali pamoja na kukuza taaluma ili waweze kusonga mbele katika sekta ya elimu Halmashauri ya Bagamoyo.