Na Raphael Okello, Timesmajiraonline,Mwanza.
WAPENZI soka mkoani Mwanza wamepongeza timu ya Pamba Fc kupanda ligi kuu bara msimu ujao wa mwaka 2024/ 2025.
Wakipokea timu hiyo ya Pamba Fc leo Aprili 30,2024 kutoka jijini Arusha wapenzi wa soka jijini hapa walijitokeza kwa wingi huku wakimwagia sifa uongozi wa timu na wachezaji wake.
Pia wamepongeza viongozi wa halmashauri ya jiji la Mwanza,Mkuu wa Mkoa huo Said Ntanda pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Amos Makalla, wananchi na wafanyabiashara, kwa ujumla kwa kuunga mkono timu hiyo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari washabiki wa mchezo wa mpira wa miguu waliwamwagia pongezi, aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais Dkt. Samia kuwa Katibu wa itikadi ,mafunzo na uenezi wa CCM taifa.
Wamesema kuwa Makalla alichangia mafanikio ya Timu ya Pamba Fc na kutoa rai kwa mkuu wa mkoa wa sasa Saidi Ntanda kuendeleza juhudi hizo.
Aidha walimtaja aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Aron Kagurumjuli kwa ushirikiano kati yake na Pamba Fc kwa kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri na na kupanda ligi kuu toka ligi daraja la kwanza.
Afisa habari wa Timu ya ya Pamba Fc Martin Mgono Sawema amesema kuwa Mafanikio yote yametokana na nia pamoja na Dhamira ya Mkoa wa Mwanza kutaka kuwa na timu inayocheza ligi kuu
Amesema mkoa wa Mwanza utahakikisha kuwa Pamba inaingia katika Ligi kuu kwa kishindo na kuleta mwamko wa pekee katika ligi kuu Bara, 2024/2025.
More Stories
ITA chatakiwa kutoa mafunzo ya viwango vya juu na kasi ya maendeleo ya Kisayansi
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake