Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi zote nchini zinazolisha watu wengi kuanzia 50 xianze kubadilisha teknolojia ya kupikia kwa kutumia nishati safi ili kukabaliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti huju akisema ifikapp mwishoni mwa 2024 Serikali inataka kuona asilimia 99 ya Taasisi za aina hiyo zinatumia Nishati Safi ya Kupikia.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati akifunga maonesho ya wiki ya Nishati yaliyofanyika Bungeni jijini Dodoma kuanzia Aprili 15 na kuhtimishwa April 19 meal hui.
Amesema kwa taasisi zote ambao bado zinatumika kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia ,zianze kubadilisha mifumo hiyo ili kwenda kwenye matumizi ya nishati mbdala.
Amesema kutumia Nishati Safi ya Kupikia na ifikapo mwisho wa mwaka 2024
ametoa maagizo kwa Wizara ya Nishati na Taasisi zake kuendelea kuboresha maonesho hayo na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha ameitaka Wizara ya Nishati kuweka mkakati wa kuhakikisha maonesho hayo yanakuwa endelevu ili wabunge wapate fursa za kuwasilisha hoja zao moja kwa moja kwa wataalam na kupewa majawabu ya hoja na changamoto zinazowakabili wao na wananchi wanaowakilishwa lakini pia ameagiza maonesho hayo yafanyike kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na halmashauri ili yale yanayofanyika Makao Makuu yabaki kuwa ya Kitaifa.
Vilevile Waziri Mkuu ameitaka Wizara isimamie na kuondoa mlundikano wa maombi ya kuunganisha umeme kwa wananchi na TANESCO ihakikishe inaimarisha mfumo wa kupokea maombi na kutekeleza maombi hayo kwa haraka.
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati kwa utendaji kazi wake ambao umechochea hali ya upatikanaji umeme nchini kuongezeka na kutosheleza mahitaji na pia kuwezesha upatikanaji wa umeme wa ziada.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuendelea kuboresha utoaji huduma ya umeme nchini.
“Tunafanyakazi kubwa kubadilisha taswira ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake na niwashukuru sana watendaji wa Wizara hii na Taasisi zake kwa kufanyakazi kwa juhudi na niwaombe waongeze kasi.” Amesema Dkt. Biteko
Amewapongeza wakandarasi wa umeme kwa kuendelea na utekelezaji wa miradi ya nishati katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na kuvipongeza vyombo vya habari nchini kwa kuendelea kutangaza habari zinazohusu masuala ya nishati kwa lengo la kujibu hoja na maswali mbalimbali ya wananchi.
Kwa upande wake, Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa sekta ya nishati ni moja kati ya sekta mtambuka nchini inayochagiza maendeleo ya Sekta nyingine na kwamba ili maendeleo yapatikane sekta ya nishati ina mchango mkubwa.
Ameeleza mchango sekta ya umeme hauepukiki katika ngazi zote kuanzia vitongoji hadi Taifa huku sekra ya uzalishaji ikiwemo viwanda na migodi na maeneo mbalimbali huku akisisitiza kuwa umeme usitumike kwa ajili ya mahitaji ya awali pekee kama kuwasha taa na kuchaji simu.
Akizungumzia mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) amesema, licha ya kuzalisha umeme Bwawa hili litasaidia masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa maji hasa mikoa ya karibu na bwawa hivyo badala ya maji kupita tu kwenye mkondo wa maji basi yahifadhiwe kwa ajili ya kusambaza kwa wananchi.
Aidha, Spika Tulia ameishauri Serikali kuanzisha gridi ya maji kama ilivyo gridi ya umeme ambayo ipo katika maeneo mengi nchini ili kusaidia usambazaji wa maji katika maeneo kame kwa kutumia gridi ya maji.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo ameipongeza Wizara ya Nishati kwa kuandaa maonesho ya Wiki ya Nishati ambayo yametoa fursa kwa Waheshimiwa Wabunge na wananchi kupata uelewa kuhusu utekelezaji wa kazi zinazofanywa na Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake na kushauri maonesho hayo kuwa endelevu.
Amesema Kamati yake itaendelea kushauriana na Wizara katika masuala mbalimbali yanayohusu nishati ikiwemo upelekeji wa huduma kwa wananchi wanaozunguka miradi mbalimbali hasa ya Gesi Asilia ili maisha yao yaendane na thamani ya miradi hiyo.
Awali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema kuwa Wiki ya Nishati kwa mwaka 2024 imekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya Waheshimiwa Wabunge na wageni mbalimbali.
Xxxxx
More Stories
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa
Zaidi ya wananchi 32,000 Vijiji vya Wilaya za Morogoro na Mvomero kuanza kupata mawasiliano
Wafanyabiashara waomba elimu ya namna watakavyorejea soko kuu