November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Buriani Mzee Mwinyi

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amefariki dunia katika Hospitali ya Mzena, jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kifo cha mzee Mwinyi kilitangazwa jana na Rais Samia Suhulu Hassan, akisema kwamba kifo chake kilitokea saa 11,30 jioni kwenye hospitali hiyo, ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya saratani ya mapafu.

Amesema Mzee Mwinyi alikuwa akipatiwa matibabu ya mapafu tangu Novemba, mwaka jana jijini London, Uingereza na baadaye kurejea nchini na kuendelea na matibabu katika Hospitali ya Mzena hadi jana, alipokutwa na mauti.

Rais Samia alisema kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo mkubwa kwa Taifa.

Aidha, Rais Samia alitangaza siku saba za maombolezo, ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kwa siku saba kuanzia leo. Alisema Mzee Mwinyi atazikwa Machi 2, mwaka huu aya Tanzania

Mwinyi alikuwa Rais wa awamu ya pili akichukua kiti hicho kutoka kwa Rais wa Awamu ya Kwanza Hayati Mwalimu Julius Nyerere baada ya kung’atuka.

Rais Mwinyi maarufu kwa jina la mzee ruksa atakumbwa kwa uongozi wake uliotukuka na madhubuti kwa kipindi chake chote cha miaka kumi, ambapo aliweza kufungua fursa mbalimbali kwa Watanzania kupitia falsafa yake ya ruksa.