January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi:Msiwatumikishe watoto kwenye uvuvi, wapelekeni shule

Judith Ferdinand, Timesmajira Online,Mwanza

Polisi Kata ya Buleji imewataka wananchi wa kijiji cha Mwalogwabagole, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto kwenye shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na uvuvi na badala yake wawapeleke shule kwa manufaa ya baadae.

Wito huo umetolewa Februari 29,2024 na Polisi Kata wa Kata hiyo ya Buleji Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (A/Insp) Gaidon Noah alipowatembelea wananchi hao kwa ajili ya kuwapa elimu ya usalama sambamba na kuwaeleza madhara ya uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.

Noah amewahimiza wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa usalama na maendeleo ya taifa.