November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Nishati yafunda viongoziwa dini, yahimiza matumizi ya gesi

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

WIZARA ya Nishati imewaomba viongozi wa dini kushiriki kikamilifu kuendelea kuihamasisha jamii kutunza mazingira kwa kuacha kutumia kuni na mkaa na badala yake kujikita katika kutumia nishati safi ya kupikia.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga wakati wa hafla ya ugawaji mitungi 1,000 ya gesi ya Oryx pamoja na majiko yake yaliyotolewa kwa viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali na wajasirianali mkoani Kilimanjaro.

Akikafafanu zaidi wakati akikabidhi mitungi hiyo iliyotolewa na Oryx kwa kushirikiana na Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Shally Raymond , Naibu Waziri Kapinga amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kusaidia jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuachana kutumia kuni na mkaa.

“Unaweza kutafakari na kujiuliza kwa nini Mbunge Shally Raymond na Kampuni ya Oryx wameamua kuwaita viongozi wa dini kuhamasisha utunzaji mazingira? Ni kwa sababu viongozi wa dini ni watu wa thamani sana.

Mjasiriamali Manka Snacks Sophia Makundi akitoa huduma ya chakula kilichopikwa kwa jiko la gesi ya Oryx wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia 1,000 ya Oryx kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro

“Unajua sisi binadamu watu ambao tunawathamini na kuwasikiliza ni viongozi wetu wa dini na mimi kwa utashi wangu mdogo naamini tunawasikiliza viongozi wa dini kwa sababu kazi ya kueneza neno la Mungu hakuna anayelipwa.

“Kwa maana hiyo ndio maana mama Shally pamoja na makundi mengine yote aliamua kuleta viongozi wa dini kwa kuwa sisi tunawaheshimu ,tuna matumaini makubwa na viongozi wa dini.

Tunaamini viongozi wa dini ndio ambao wanaweza kutusaidia kuwaelimisha na kuwaambia wananchi kuhusu kutunza mazingira,”amesema Naibu Waziri Kapinga.

Pia amesema kuwa katika kampeni hiyo ya kuhamasisha matumizi ya nishati ya kupikia wamekuwa wakihusisha zaidi wanwake kwasababu wanawake ndio wanaokaa jikoni kupika kuandaa chakula.“Kwahiyo mwaka 2024 tusikubali kupika kwa kuni wala mkaa.

Akizungumzia kampeni ya nishati safi ya kupikia, Naibu Waziri Kapinga amesema mwaka jana mwishoni kulikuwa kuna mkutano wa dunia wa mazingira na katika mkutano huo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alienda na ajenda mahususi ya kumkomboa mwanamke wa Afrika sio mwanamke wa Tanzania peke yake.

“Kumkomboa vipi? Kuweka mikakati ya kuhakikisha wanawake wote wa Afrika wanatumia nishati safi ya kupikia na katika mkutano ule ulihusisha wakuu wa nchii.

Rais Dkt. Samia kutokana na umahiri wake na uwezo wake aliweza kukusanya viongozi na kuzindua program maalum kusaidia wanawake wa Afrika kwenye kutumia nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania, Shaban Fundi aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Benoite Araman, ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wanajivunia kuwezesha makundi mbalimbali yakiwemo wanawake, watoto na wajasiriamali kupata nishati safi ya kupikia.

Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga (wa tatu kushoto) akiwa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo (wa kwanza kushoto) Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Shally Raymond ( wa pili kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro (wa pili kulia) na Meneja Masoko wa Oryx Shaban Fundi (wa kwanza kulia) wakati wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx, Sister Piala Olomi kutoka Shirika la Masisita wa Bibi Yetu Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 1,000 ya kupikia ya Oryx kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wajasiriamali Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Polisi (CCP) mkoani Kilimanjaro. Na mpiga picha wetu.

“Kufanya hivyo tunaamini tunaikomboa jamiina taifa kwa ujumla wake kwani kupika kwa gesi ya Oryx kuna maanisha kuboresha afya za kinamama kwa kueuka kuvuta moshi mbaya wa kuni na mkaa.Pia tunaweza watoto kupata muda wa kwenda shule badala ya kutumwa kutafuta kuni,”amesema Fundi.

Amesisiza kampuni hiyo kwa kutambua nafasi ya viongozi wa dini imeona ni vema sasa ikatoa mitungi ya gesi ya Oryx na majiko yake kwa kundi hilo sambamba na kuelezea kwa kina umuhimu wa kutunza mazingira na wanaamini kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kusema na kusikilizwa, hivyo watakapokuwa mabalozi wa kuzungumzia nishati safi ya kupikia jamii itabadilika na hivyo kuokoa mazingira.

Aidha, amekumbusha kuwa mwaka 2021 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alianzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia na alitoa maono yake ya kwamba ifikapo mwaka 2032 asilimia 80 ya wananchi itumie nishati safi, hivyo kuanzia hapo Oryx iliongeza nguvu na hadi sasa ya mitungi 19000 bure yenye thamani isiyopungua Sh.bilioni 1.5.