November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Walimu wa madarasa ya awali wahimizwa kuwalinda watoto

Na Joyce Kasiki,Dodoma

NAIBU Katibu Mkuu Prof.James Mdoe amewataka walimu wanaofundisha maradasa ya awali kuhakikisha wanawalinda watoto dhidi ya aina mbalimbali za ukatili.

Prof.Mdoe ameyasema hayo Feb 22,2024 jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa walimu wa madarasa ya awali katika mkoa wa Dodoma ambayo yamelenga kuwapa ujuzi wa kufundisha madarasa hayo ikiwa ni pamoja na kumudu madarasa hayo ambayo mara nyingi yanakuwa na watoto wengi darasani.

Amesema,watoto wanaosoma katika madarasa hayo wamekuwa wakikutana na kadhia mbalimbali wakati wa kwenda shuleni,kurudi nyumbani lakini pia wamekuwa wakikumbanana kadhia hizo nyumbani.

Mkurugenzi wa CiC Craig Ferla

“Lakini ninyi kama walimu mna jukumu la kuwalinda watoto ili kuwakinga dhidi ya changamoto za ukatili zikiwemo za unyanyasaji wa kingono wanaofanyiwa majumbani ,njiani wakati wa kwenda shule,shuleni kwenyewe ambapo kuna watumishi wasio waaminifu wamekuwa wakifanya vitendo vya ukatili kwa watoto.”amesema Prof.Mdoe

Amesema walimu hao wanapaswa wawe marafiki wa watoto hao ili wawe wawazi kwao na waweze kuwaeleza madhira wanayokumbana nayo hasa ya ukatili.

Aidha amewaasa walimu hao kutumia mafunzo wanayopatiwa ili yakawe chachu ya kuhakikisha watoto hao wanakua katika utimilifu wao na hivyo kuwa tija kwa Taifa hapo baadaye.

“Kwa mujibu wa sensa ya 2022,kuna watoto karibu milioni 16 ambao wapo wenye ngazi ya kupata elimu ya awali,hii ni rasilimali muhimu kwa ujenzi  wa Taifa letu na ndio maana naiita hazina,tukikosea kuwaandaa sasa hawa mil 16 wakija kuwa watu wazima huwezi kuwategemea katika kujenga uchumi”amesema Prof.Mdoe na kuongeza kuwa

washiriki wa mafunzo ya elimu ya darasa la awali

“Kwa maana hiyo tuna kazi kubwa ya kufanya sasa kuwaanda ili wawe tayari na tuweze kupata watanzania walioelimika na ambaye yupo tayari kwa ajili ya ujenzi wa Taifa lake.

Ametumia nafasi hiyo kulishukuru shirika lisilo la kiserikali linaloshughulia a masula ya watoto wadogo (CiC) kwa namna linavyoshiriki katika suala zima la uboreshaji wa elimu nchini .

Kwa upande wake Murugenzi wa CiC Craig Ferla amesema ,CiC inaamini kwamba mtoto akikua katika utimilifu wake Taifa nalo  litakua kwa utimiifu wake.

Hata hivyo ameishukuru seriakali ya awamu ya sita kwa kuwekeza katika  elimu ya awali ambayo imeingizwa kwenye elimu ya msingi na inapatikana bila malipo ambapo watoto zaidi ya mil 1.5 wanapata fursa ya elimu ya awali kila mwaka.