October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa Ushirika wa wafugaji wa ng'ombe Wilaya ya Kinondoni,Kajia Mrita akionyesha moja za mashine za usindikaji wa maziwa zilizopo katika banda la uvuvi na Mifugo katika maonesho ya 44 ya kimataifa ya Biashara sabasaba

Wafugaji Kinondoni waomba kukopeshwa mashine za usindikaji maziwa

Na Penina Malundo,Times Majira Online, Dar es Salaam

WAFUGAJI, Ng’ombe wa maziwa wilaya ya Kinondoni, wameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi nchini pamoja na Bodi ya Maziwa kuwasaidia kuwakopesha mashine za usindikaji maziwa.

Ombi hilo lilitolewa leo jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba na Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafugaji hao, Kajia Mrita.

Akitoa ombi hilo Mrita amesema, hali ya uzalishaji wa maziwa katika wilaya yao ipo juu ukilinganisha na miaka ya nyuma hivyo uongezwaji wa thamani na usindikaji wa maziwa utaweza kuwafanya kuuza maziwa kwa bei nzuri kuliko sasa.

“Tutakapo saidiwa mashine hizi na serikali tunaamini kwa kiasi kikubwa tutasindika maziwa haya, na kuyafanya kuwa na bei nzuri zaidi kuliko vile tunapokamua na kuuza moja kwa moja,”amesema na kuongeza.

“Mashine hizo zilizopo katika maonesho hayo yenye ujazo wa lita 200 hadi 500 endapo tutapata mashine hizi tunaamini soko la maziwa litazidi kuongezeka,”amesema.

Amesema, ni vyema serikali ingewasaidia kupata mashine hizo ili ziweze kuwasaidia katika ufugaji wao.