Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Chama Cha Mapinduzi nchini Tanzania (CCM) kimeahidi kumsomesha mtoto Alhaj Abdallah, anayefanya biashara ya kuuza ndizi mbivu mjini Kigoma ili kuweza kumuhudumia mama na wadogo zake.
Ahadi hiyo ilitolewa jana na Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi baada ya kusikia maelezo ya mtoto huyo ambaye amekuwa miongoni mwa waliokuwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma Mjini.
Katika maelezo yake Mwenezi Makonda alisema Chama Cha Mapinduzi kimempa Mama wa Alhaj mtaji wa kufanya biashara pamoja na kugharamia matibabu yake ya tumbo.
“Acha sisi tumsomeshe, tutatafuta viongozi waende kwa mama alafu tutampeleka mama hospitali, Chama kitamgaramikia mama, utasomeshwa na Chama Cha Mapinduzi na mimi ndiyo kaka yako na leo biashara ya ndizi inaishia hapahapa, wewe siyo masikini kuanzia leo na mama tutampa kodi”
“Nampa mkuu wa Wilaya ela ya kulipia Kodi ya nyumba ya mwaka mzima na kesho atafute shule, tunampa mama ela ya Mtaji afanye biashara, na wewe uwe unaenda shule, na mkuu wa Wilaya atakua anafatilia ” Makonda alimweleza mtoto huyo.
Mtoto Alhaj alimueleza Mwenezi Makonda kuwa mama yake mzazi amekuwa akisumbuliwa na uvimbe wa tumbo pamoja na umaskini wa kutopea kutokana na mama yake kutokuwa na biashara ya kufanya.
“Mimi nauza ndizi, Mama yangu alivimba tumbo alikua anaumwa, sisi tulikua waislam, nikamshauri mama aende kwenye kanisa la Sayuni, Mungu akamjalia akawa anapona kidogokidogo, nikamwadisia mtu, akanisaidia Elfu nne akasema nikanunue mboga tule lakini nilijituma nikafanya biashara, nikaenda kununua ndizi nikauza nikapata Elfu 20, tukaenda kupanga nyumba”
“Ikafika muda tukawa tunadaiwa kodi, mama akaniambia, mwanangu, Si unaona mama yako naumwa, na tu adaiwa Kodi, nikachukua Elfu 20 ili alipe kodi, nilivyolipa Kodi, kuna watu wananijua, nikasema hapa nitapata biashara wapi? Nikaenda kuwahadisia wale wanazareti wakasema chukua biashara (ndizi) hii ukishauza utarudisha pesa”
Mtoto huyo aliongeza kwa kusema”Mimi namlisha mama na wadogo zangu, mimi ni mtoto wa pili na dada yangu tulikua tunakaa nae hapohapo masanga, mtu akaja akamtafutia kazi Tabora, na anamiaka 14, alikaa kidogo na amesharudi nyumbani kigoma, shida yangu naomba unisaidie unisomeshe shule yoyote
Ili nimsaidie mama yangu”
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba