November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

CCM yatoa siku 14 Jiji la Mbeya kumaliza tatizo la taka

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya kimetoa siku 14 kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuhakikisha taka zote zinazozagaa mitaani zinaondolewa mara moja .

Mwenyekiti Chama Cha Mapinduzi Patrick Mwalunenge

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya , Patrick Mwalunenge wakati akisilikiliza kero za wananchi ikiwa ni maadhimisho ya miaka 47 tangu kuzaliwa kwa chama hicho.

“Nitapita Mwenyewe na kamati yangu mtaani kuangalia taka hizo mitaani kwa wananchi katika hizo siku 14 nilizotoa,sitapenda kuona taka zikizagaa tena,”amesema Mwenyekiti wa Chama hicho .

Laiton Mwakibete Mkazi wa Soweto jijini Mbeya amesema kuwa suala la taka ni changamoto kubwa kwa Mkoa wa Mbeya hali inayowafanya wananchi kuishi nazo katika nyumba zao baada ya kuondolewa kwa maguba ya taka imekuwa kero kubwa kwenye makazi ya watu.

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,John Nchimbi

“Hivi sasa zimeelekezwa kwenye mito mvua zikinyesha taka zinatupwa ovyo kwenye mito hiyo na nyakati za usiku kutelekezwa kwenye makazi ya watu hivyo kuwa kero kutokana na kukithiri kwa uchafuzi,”amesema.

Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,John Nchimbi amekiri uwepo wa taka hizo na kusema kuwa hali ilisababishwa na upungufu wa nyenzo yakiwemo magari.

Hata hivyo amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo halmashauri imetoa zabuni kwa shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT) kuongeza nguvu ya kuondoa taka katika kata tano za halmashauri hiyo na kwamba akionesha ufanisi atapewa jukumu hilo kwenye kata zote.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge hayupo pichani