November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba mzazi awapa tabasamu walimu na watumishi

Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya

MKURUGENZI wa shule ya Holyland Pre& Primary School  iliyopo katika Mji mdogo wa Makongolosi wilayani Chunya mkoani Mbeya, Lawena Nsonda (Baba mzazi )amewapatia zawadi walimu  na watumishi wa shule hiyo baada ya  wanafunzi wa darasa la Nne (4)kufanya vizuri mtihani wa Taifa kwa kuwa na matokeo mazuri kwa miaka mitatu mfululizo.

Amesema kuwa amechukua uamuzi huyo kutokana na kuthamini mchango mkubwa wa walimu na watumishi wote wa shule katika suala Zima la usimamiaji mzuri wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na ufundishaji mzuri wa wanafunzi wa darasa la nne (4) ambapo shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo.

Nsonda amesema hayo wakati wa hafla ya kuwapongeza walimu na watumishi wote wa shule hapo   lengo likiwa kuwathamini na kuwapa moyo wa ufundishaji na malezi  Bora ya watoto hao .

“Nimeamua kufanya hafla hii  si kwa walimu tu bali nimewaunganisha na watumishi wengine ambao sio walimu sababu Hawa watoto hawawezi kufanya vizuri bila kula vizuri,ulinzi ,na vitu vingine muhimu maana Mimi na walimu na watumishi wengine hapa shule ni cheni moja ndo maana sababu ya kuwa elimu yetu ipo vizuri Sana na ndo sababu ya kuongoza kitaifa kwenye matokeo yetu ya darasa la nne ya watoto wetu hapa kuanzia mkurugenzi wa shule kuna ushirikishwaji kuanzia ngazi ya chini kabisa “amesema Nsonda.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa Mwalimu ni mtu Muhimu sana ndo sababu amekuwa akiwapa motisha na hata pale wanapokuwa na changamoto mbali mbali amekuwa akifanya mazungumzo nao lengo likiwa ni kuwafanya kuwa na mawazo  ili waweze kufanya Kazi pasipo kuwa na mawazo hali kadhalika hata kwa watumishi wengine ambao sio walimu.

Gladness Malakasuka ni Mwalimu wa shule hiyo amesema kuwa kitendo ambacho mkurugenzi huyo anafanya kwa walimu na watumishi kinaleta faraja na moyo wa kufanya kazi vizuri kutokana na kuthamini watumishi wake wamiliki wengine wakiiga mfano wa mkurugenzi huyo watoto wengi watakuwa wakifanya vizuri katika masomo yao.

Naye Haruni Malambugi ambaye ni mwalimu madarasa ya awali Holyland amesema kuwa mkurugenzi huyo ni mfano wa kuigwa Sana kwani ni wamiliki wachache wanaofanya hivyo kwa watumishi na walimu katika kuwathamini na kuwatia moyo katika suala zima la ufundishaji na ufanyaji kazi.

Shule ya Holly Land  iliyopo wilayani Chunya mkoani Mbeya imekuwa na matokeo chanya ambayo imechangiwa na miundo mbinu rafiki ya shule ambayo inawawezesha wanafunzi kusoma bila vikwazo.