Na Jackline Martin, TimesMajira Online
KAMPUNI ya michezo ya kubashiri Betika, kwa kushirikiana na Tigopesa imewapeleka mabingwa wawili wa kwanza wanaoelekea nchini Ivory Coast, kushuhudia Michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023), lengo likiwa kuiunga mkono timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika michuano hiyo.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa Kampuni hiyo, Juvenalius Rugambwa amesema washindi hao walipatikana kupitia kampeni ya ‘Twenzetu Ivory- Coast ki-VIP’ wamegawanywa katika makundi mawili ili watu wapate fursa ya kutazama burudani mbalimbali.
Kundi la kwanza kati ya hao, watatazama mechi ya Morroco dhidi ya Tanzania na kundi la pili watasafiri Januari 20, kutazama mechi kati ya Tanzania dhidi ya Zambia.
Amesema, jumla ya washindi watakuwa 6, na kwa sasa watatangulia washindi wawili na awamu ya pili wataenda wanne.
Pia, amesema Betika imegharamia Kila kitu katika promosheni hiyo kwa kushirikiana na kampuni kubwa ya mitandao ya simu ya Tigo kupitia Tigopesa.
“Betika pamoja na Tigo inakwenda kusimamisha Abijan na hii ni katika promosheni yetu ya “Twenzetu Ivory -Coast Ki-VIP” amesema.
Kwa upande wake mshindi wa Promosheni hiyo, Elius Simba ambaye ni mkazi wa Kigoma, amesema amepokea kwa furaha ushindi huo na amepata ushirikiano mzuri kutoka kwa Betika hadi kufikia kuanza safari yake ya kwenda kushuhudia mechi hiyo
“Nimepokea kwa furaha sana tangu siku ya kwanza nimetangazwa, ushirikiano ulikua mzuri kati ya Betika na mimi hivyo nimejiandaa kwenda kuiunga mkono Stars, nchini Ivory Coast na naamini katika mechi ya kwanza tutatoka na ushindi mnono,” amesema.
Naye mshindi mwingine, Nassib Staphord amesema ushindi huo aliupokea kwa furaha kwa sababu ni kitu ambacho kinakwenda kuweka alama mpya kwenye maisha yake kwani hajawahi kwenda kuangalia mechi ya Afcon Live nchi za nje.
Ameongeza kuwa, wao kama watanzania wanaenda kuongeza nguvu kwa watanzania wengine ambao walitangulia na wanatarajia kurudi wakiwa na ushindi mkubwa.
Jinsi walivyoshiriki washindi hao ni kuweka pesa kwenye akaunti ya BETIKA kupitia Tigo Pesa na kusuka mikeka na kuingia kwenye droo ya ushindi
Sambamba na Hilo BETIKA inaendelea kutoa TV inch 70 na king’amuzi kilicholipiwa mwezi mzima buree.
Kubeti www.betika.co.tz au piga 14916#
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania