Na Mwandishi wetu, timesmajira
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) linatarajia kuonesha na kutangaza michuano ya Mpira ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024 ambayo itafanyika nchini Ivory Coast mwaka huu.
Michuano hiyo itaoneshwa bure kupitia katika chaneli zote za TBC1, TBC2, na mtandao ya YouTube wa TBC online pamoja na Redio ambayo inatarajiwa kuanza Januari 13 huku fainali kuchezwa Februari 11 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Januari 9, 2024 Mkurugenzi Mkuu TBC, Dkt Ayub Rioba amesema ni jukumu la msingi na ni dhima ya TBC kama chombo cha umma kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na furaha itokanayo na burudani hususani za kimichezo.
“Sisi kama chombo cha taifa tuna dhima, tuna jukumu, la msingi la kuhakikisha tunawaletea Watanzania furaha hasa kwenye michezo na ndio maana kwa mujibu wa taratibu za FIFA na hata CAF ni kwamba michezo hii mara nyingi inapelekwa kwenye chombo cha habari cha umma,” amesema Dkt.Rioba
Amesema wakati wa michuano hiyo ikiendelea kutakuwa na uchambuzi ambao utakuwa ukifanywa na wataalamu ambao ni waandishi wa habari.
“TBC tumejitahidi kuboresha maudhui yetu sasa hivi tupo “FULL HD” visimbuzi vyote lazima TBC iwepo atazame bure mechi hizi sio za kukosa “amesema na kuongeza kuwa
“Mbali na kuwepo na uchambuzi pia kutakuwa na vipindi vya katikati ambavyo vitakuwa vikifanya uchambuzi wa masuala mbalimbali katika michuano hiyo”amesema Dkt Rioba
Vilevile amesema michuano hiyo imebeba ujumbe mahususi wa kipute mseleleko ambapo amewahakikishia watanzania kuwa mda wote wataweza kuona michuano hiyo hata kama wamelipia kizimbuzi au awajalipia”amesema Dkt Rioba
Aidha amesema kuwa TBC ina watangazaji mahiri wenye vipaji vya uhakika visivyokuwa na ubabaishaji.
“Kuanzia enzi hizo ikiwa RTD hadi miaka ya sasa tuna watangazaji mahiri sana, tunaibua vipaji kila mwaka tuna watu mahiri kwelikweli, kuna wakati watu wanadhani ubunifu ni ule ubabaishaji, mbwembwe za kibabaishaji, hapana, TBC tuna vijana mahiri amesema Dkt. Rioba.
Aidha amewaomba wadau kujitokeza kutangaza katika mechi hizo kwani sio za kukosa ili waweze waweze kuendelea kuziona katika ubora zaidi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi