November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya twenzetu darasani 2024 kuwafikia watoto 4500

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Raoma Foundation kupitia Kampeni yake ya Twenzetu darasani 2024 mafanikio ya mtoto darasani yanaanza na mimi imejipanga kuwafikia watoto wenye mahitaji maalumu na wanaoishi mazingira magumu 4500 kwa kuwapatia vifaa mbalimbali shule.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Januari 6, 2024 Mkurugenzi mwenza wa taasisi hiyo Rahma Abdallah wakati akitoa taarifa ya mwendelezo wa kampeni ya Twenzetu darasani 2024 amesema kampeni hiyo imelenga kufikia mikoa saba katika hatua za awali.

Mkurugenzi mwenza wa Taasisi ya Raoma Foundation, Rahma Abdallah akizungumza na waandishi wa habari katika hafla hiyo

Abdallah amesema taasisi hiyo imeamua kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia watoto mahitaji mbalimbali.

“Kampeni hii imelenga kushirikiana na Serikali katika kutoa vifaa vya shule Kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu na wanaoishi katika mazingira magumu,” amesema Abdallah

Amesema kampeni hiyo itafanyika Tanzania Vara na Visiwani ambapo kwa kuanzia itaanza Kizimkazi Zanzibar na baadae Pwani, Lindi, Singida, Dodoma pamoja na Mtwara.

Aidha amewaomba wadau wengine kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi ambazo amekuwa akizifanya katika sekta ya elimu.

Pia ametoa wito kwa wazazi na walezi kujitokeza kuwaandikisha shule kwani jukumu na maono ya mtoto yanabebwa na mzazi.

Kwa upande wake Mratibu wa kampeni hiyo Meshack Mafyeko amesema kampeni hiyo itadumu ndani ya mwaka mmoja ambapo taasisi hiyo itakuwa ikitembelea shule katika maeneo husika ili iweze kuwabaini watu husika.

“Taasisi ya Raoma imejipanga na tupo tayari kufanya kazi kwa asilimia 100 hivyo tunawaomba wadau, wazazi kuunga mkono Serikali ili watoto waweze kupata elimu bora na kuepuka chagamoto wanazozipata katika mazingira ya shule,”amesema Mafyeko.

Mdau wa Taasisi hiyo , William Lyangoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Kampeni ya Twezentu darasani 2024

Aidha aliipogeza Serikali Kwa kuendelea kutoa fedha Kwa ajili ya ujenzi wa shule na kuhaidi kuwa taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Serikali.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kampeni hiyo mdau wa Raoma Foundation, William Lyangoo amesema taasisi hiyo imekuja kama chachu kuinga mkono Serikali katika kuwapatia nyezo wanafunzi.