Na Agnes Alcardo, Timesmajira, Online. Dar
BODI ya Wakurugenzi ya Kampuni Tanzu ya Mafuta (TANOIL) ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Menejimenti ya kampuni hiyo, wameaswa kuhakikisha wanaimarisha na kuleta matokeo chanya kiutendaji kwa watanzania na Taifa kwa ujumla.

Hayo yameelezwa Januari 5, 2024 na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alipofanya ziara ya kikazi katika kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam.
Ambapo ameieleza bodi na menejimenti kuwa wahakikishe TANOIL inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo, dhima na adhima ya kuanzishwa kwa kampuni hiyo nchini.
Vilevile ameelekeza kuwa viongozi hao watumie mbinu zao,taaluma na uwezo wao wote kuhakikisha kampuni hiyo inatengeneza faida zaidi badala ya hasara kwa taifa na waepuke kuzalisha madeni.

Pia Judith, ameielekeza TANOIL kushirikiana na TPDC, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika kutekeleza majukumu yao kwa kuwa yanashabiliana ili kuleta matokeo chanya ya kampuni hiyo katika kujiendesha.
More Stories
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya
Kenya,Uganda zaanzisha mradi wa uendelezaji rasilimali za maji Angololo