Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro
Katibu wa Chama Cha wachimbaji Mkoa wa Manyara ( MAREMA ) Tawi la Mirerani Rachel Njau amesema Chama Cha wachimbaji Tawi la Mirerani limetoa Mapendekezo kuwa mgogoro wa mitobozano ya mipaka baina ya Kampuni ya Franone Mining na wachimbaji wadogo utatuliwe bila kuathiri upande wowote.
Hayo ameongea hivi Karibuni wakati akizungumza na Majira mara baada ya kuhitimusha mkutano wa mwisho wa Mwaka wa Chama Cha wachimbaji Mkoa wa Manyara Tawi la Mirerani ulifanyika katika ukumbi wa Songambele Mji Mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.
Njau amesema Chama kimependekeza kuwe na rasimu itakayotumika kutatua Migogoro midogo na kamati za usuruhishi migodini ipewe meno ili iweze kusuluhisha pia mitobozano au changamoto za wachimbaji wakubwa, hii itasaidia katika kuondokana na Migogoro iliyoko ndani ya ukuta wa Magufuli.
Aidha amesema kuwa Migogoro hiyo itatuliwe lakini lengo kuu likiwa ni kuhakikisha Mwekezaji wa Kampuni ya Franone Mining na wachimbaji wadogo pande zote mbili ziweze kuwa salama bila kuasili upande mmoja.
” Chama kimependekeza kuwe na rasimu itakayotumika kutatua Migogoro midogo na kamati za usuruhishi migodini ipewe meno ili iweze kusuluhisha pia mitobozano au changamoto za wachimbaji wakubwa, hii itasaidia katika kuondokana na Migogoro iliyoko ndani ya ukuta wa Magufuli” amesema Katibu wa MAREMA Tawi la Mirerani Rachel Njau.
” Tulikua na changamoto mbalimbali kama mlivyosikia katika mkutano wetu wa mwisho mwa mwaka kuwa wachimbaji wadogo wa mpakani wana changamoto na Mwekezaji lakini kama Chama tumeomba tupewe au tumuombe RMO na Mwekezaji aliyepo na wale wenye changamoto nao tukae tuzungumze, kwasababu masuala ya mpakani hayajaanza leo ni changamoto ya muda mrefu, na safari hii Mwekezaji aliyekuwepo ni Mtanzania na alikua mchimbaji mdogo na nina uhakika ni msikivu na mzalendo, tuweze kujua nini tunaweza kufanya ili tuweze kuwa salama pande zote mbili bila kuasili upande mmoja” anasema Rachel Njau.
Hata hivyo Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Mirerani Jumanne Athuman Nahe anasema RMO Nchagwa amealikwa Mgeni rasmi katika mkutano huo na amefafanua vizuri juu ya Kitalu C na wachimbaji wadogo Kwa lengo la kupata muafaka wa jumla.
Nahe anaongeza anaimba serikali na Bunge kuhakikisha inabadilisha Sheria ya Vertical hasa hasa kwa eneo la Mirerani kwasababu Tanzanite inachimbwa kutokana na ulalo wa Mwamba unakoelekea.
” Sasa sisi kama wadau na viongozi wa vyama vya Wachimbaji tunaiomba Serikali ishirikiane na wadau na wachimbaji katika kuhakikisha inasikiliza kero za wachimbaji Kwa kutoa muafaka bila kuumiza upande mwingine” anaongeza Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Mirerani Nahe.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â