November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

ASA yatoa msaada wa chakula na mbegu za kilimo Hanang

Na Lubango Mleka, Times majiraonline – Hanang Manyara.

WAKALA wa Mbegu za Kilimo (ASA) imekabidhi Msaada wa Chakula na Mbegu za Kilimo jumla ya Tani 25 zenye thamani ya Sh.Milioni 85 kwa ajili ya Wahanga wa Mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang Kateshi Mkoani Manyara.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Msaada huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) Dkt.Sophia Kashenge amesema kuwa, ASA imekabidhi Tani Moja ya mbegu za Alizeti sawa na kilo 1000 zenye thamani ya Sh.Milioni Tano, Tani Moja ya mbegu za Mahindi sawa na kilo 1000 zenye thamani ya Sh.Milioni 3.5, Mbegu za Ngano kiasi cha kilo 15,000 zenye thamani ya Milioni 60 na Unga wa Ngano Kilo 8000, ambapo vyote kwa pamoja vina jumla ya thamani ya Milioni 85.

“Wakala wa Mbegu inaamini mchango huu utagusa jamii kubwa iliyo athirika, lengo la ASA ni kuwarejesha wapendwa Wakulima wetu shambani haraka iwezekanavyo kwa kuwapatia mbegu bora pamoja na chalula,” akisema Dkt.Kashenge.

Aidha ametoa pole kwa Serikali na kuipongeza Wizara ya Kilimo kwa kutoa maelekezo hayo muhimu kwa Wahanga wa mafuriko Kateshi Hanang.