November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chalamila azindua kadi ya Visa Tanesco Saccos

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amezindua kadi ya Visa kwa ajili ya wanachama wa Tanesco Saccos huku akisisitiza umuhimu wa kuwa waadilifu katika utendaji wa kazi zao.

Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye uzinduzi wa matumizi ya kadi hiyo yaliyoenda sambamba na mkutano Mkuu wa 55 wa Tanesco Saccos aliwapongeza kwa kuanzisha huduma hiyo ya kadi na kusema kuwa watakuwa katika hadhi ya kimataifa.

“Nadhani nyie ni Saccos ya kwanza kuzindua kadi hii, mnatoka ndani na mnaingia kimataifa niwapongeze sana kwa hilo kwasababu popote unapokuwa hata nje ya nchi mnaweza kuhamisha fedha jambo ambalo ni zuri sana na hongereni sana,”amesema.

Pamoja na hayo, Chalamila alizungumzia pia suala la uadilifu akisema wengi wanalinganisha na umaskini lakini ni suala muhimu katika utendaji kazi kuwezesha Saccos kuwa imara.

Aliwahimiza kutumia Saccos hiyo kama chanzo cha kuongeza mapato na kubadilisha maisha yao kiuchum

Naye Mwenyekiti wa TANESCO Saccos,Somoe Nguhwe amesema ni mkutano mkuu wa mwaka na tukio muhimu la kisheria lianalowakutanisha viongozi, watendaji wa Chama na wawakilishi na kutoa ripoti mbalimbali zinazoonyesha utendaji wa Chama kwa mwaka uliopita.

Amesema kupokea na kujadili taarifa ya makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024 na kupitisha maazimio kwaajili ja utekelezaji kwa mwaka fedha ujao.

“Mwaka 2022 ulikuwa na changamoto nyingi za kiutendaji iliyozalisha matokeo mchanganyiko yakiwemo hasi na chanya katika utendaji wa shughuli za chama ikiwemo changamoto ya ukwasi katika chama iliyosababishwa na kuimarika kwa wigo wa kukuopesha kwa wanachama imepelekea utoaji wa huduma za mikopo kuwa na foleni kusababisha wanachama kutofikia malengo ya mikopo,”amesema

Amesema Tanesco Saccos idadi ya wanachama imeongezeka kutoka 6063 mwaka 2021 hadi kufikia 6,354 katika mwaka uliisha ongezeko sawana asilimia 4.8.

Aidha amesema akiba za wanachama zimekua kutoka bilioni 41.9 kwa mwaka 2021 hadi kufikia bilioni 41. 1 mwaka 2022 na kufanya ongezeko la asilimia 5.2 na chama kimetoa faida juu ya akiba na hisa za hiyari kiasi cha bilioni 1.5.

“Jumla ya mkiopo yote iliyotolewa katika mwaka 2022 ilifikia bilioni 57. 1 ikalinganishwa na mwaka mwaka 2021 ilikuwa bilioni 48.9 sawa na ongezeko la asilimia 16.8, “amesema.

Amesema kuwa mpango mkakati wa chama kwa kipindi cha miaka mitano mwaka 2024/28 ikiwa ni mpango wa tatu kutekelezwa na chama umejikita kulinda na kukuza mafanikio yote yaliyopatikana katika mipango ya kabla.