Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Jumla ya vijana 818 kutoka Wilaya za Ilemela na Sengerema mkoani Mwanza wamenufaika na mradi wa Kuimarisha Ujasiriamali na Ajira kwa Vijana(EYEE) ulioanza mwaka 2021 hadi Desemba 2023.
Ambapo mradi huo unatekelezwa na shirika la Volunteer Service Overseas (VSO) na unafadhiliwa na Standard Chartered Foundation kati ya vijana hao 86 ni wenye ulemavu na 732 ni wasio na ulemavu.
Akizungumza katika kikao cha kufunga mradi kilichofanyika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ofisa Mradi wa Shirika la VSO Photunatus Nyundo ameeleza kuwa mradi huo ulilenga vijana hususani wa kike kwa asilimia 60 pamoja na wenye ulemavu asilimia 10.
“Wakati tunaanza utekelezaji wa mradi huu tulipata changamoto ya kupata asilimia 10 ya vijana wenye ulemavu ndio tukafanya hatua za makusudi kuwaleta wadau wengine katika timu yetu ili waweze kutushauri namna bora yankuwapata na kuwahudumia na mradi utakapo isha basi vyama vyao waweze kuwatumia ndio tukawaleta TAB na CHAWATA,”ameeleza Photunatus.
Photunatus ameeleza kuwa maeneo ya uwezeshaji ambayo vijana hao wamenufaika kupitia.mrafi huo ni pamoja na mafunzo mbalimbali ya kuwawezesha wajasiriamali kutoka hatua moja kwenda nyingine ikiwemo usimamizi wa biashara,fedha na wateja, kudumisha uhusiano na wateja pamoja na kuboresha ubora wa bidhaa zao.
‘Kwa sababu tunafahamu changamoto ya wajasiriamali wadogo katika kupata huduma mbalimbali tukawawezesha ili watambue umuhimu wa kurasimisha biashara zao na kuwaunganisha na wadau wanatoa huduma hizo za urasimishaji ambapo wengi wameweza kusajili TIN namba ili waweze kulipa kodi,leseni za biashara na majina ya biashara kupitia BRELA na TBS wale wenye bidhaa ambazo zinahitaji taasisi hiyo OSHA kurasimisha maeneo yao ya kazi na usalama mahali pa kazi,”anaeleza Photunatus.
Eneo la pili ni kushauri nyenzo pamoja na teknolojia kwani changamoto ambayo wajasiriamali wanakuwa nayo ni kutopata ushauri sahihi wa kuendesha biashara zao.
“Ili awe na uwezo wa kutofautisha fedha binafsi na fedha ya biashara ili aweze kujua namna bora ya kuzungumza na mteja,kutunza kumbukumbu za kifedha na biashara hivyo tukawa tunatoa huduma za ushauri,”ameeleza Photunatus.
Pia amesema wameandaa nyenzo mbalimbali za kuwasaidia wajasiriamali kutunza kumbukumbu za kifedha ambazo zinampa muongozo bora wa kuandika hesabu zake ili aweze kutambua biashara yake kama inakuwa au haikui huku akieleza kuwa wapo wajasiriamali wachache na wawakilishi wa vikundi ambao walipata fursa za vifaa vya kuzalishia bidhaa.
“Mashine mbalimbali zolitolewa chini ya mradi huu kwa wajasiriamali hao ili kuwezesha kuchangiza uzalishaji mali wao,”amesema.
Eneo la tatu la uwezeshaji ni uhusiano na soko kwani wajasiriamali wamekuwa na changamoto ya kupata soko la uhakika.
“Kupitia wataalamu wetu tumekuwa tukiwashirikisha wadau mbalimbali ili waweze kupata masoko ya uhakika ya bidhaa zao kwa kuwapeleka katika fursa kukutana na watu ambao watauza bidhaa zao kama vile maonesho,vikao vya kimkakati pamoja na mikutano ya kibiashara,”anaeleza.
Ufuatiliaji na uendelevu ambapo walipo wapa mafunzo na vifaa vya kazi hawakuishia hapo wamekuwa wakifanya ziara mbalimbali za kuwatembelea ili kujua wanaendeleaje na kuona kama wanatekeleza yake ambayo wamewafundisha kuona kama wanakuza biashara zao.
“Katika uendelevu tunafahamu miradi yetu inaenda na ukomo wa muda hivyo ni muhimu kuweka mazingira ya huduma ambazo tumewapatia zinaendelea kupatikana,tumekuwa tulifanya na taasisi wazawa SIDO itaendelea kiwepo ata kama VSO haipo Tanzania,”.
Pia katika upande wa ajira wamewezesha vijana hao mafunzo ya kuweza kujiajiri au kuajiriwa kwa kuwafundisha stadi za maisha,kutambua nini afanye,nidhamunya kile anachofanha pamoja na uongozi pamoja na elimu jumuishi pia mafunzo ya ujuzi.
Kwa upande wake Maneno Maporo kutoka SIDO ameeleza kuwa SIDO wamekuwa wakisaidia wajasiriamali wa viwanda vidogo kupata leseni na huduma kutoka taasisi zinazohusika na biashara ili kurahisisha kazi na wasipate mkwamo wowote pia ameishukuru VSO katika kipindi hicho cha miaka mitatu kuongeza nguvu kwa kundi hilo.
Katibu wa Chama cha watu Wasioona(TAB) Meshack Masanja ameeleza kuwa kumfuata mtu ambaye ameisha kata tamaa ya maisha ili awe mnufaika ni jambo gumu sana.
“Makundi ya watu wenye ulemavu hususani wasioona mkoani Mwanza hasa wale walioshindwa kupata elimu ya msingi au elimu kwa ujumla kwa bahati mbaya programu nyingi zilikuwa zina wa kwepa nashukuru VSO kwa kutukumbuka walemavu,”amesema.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Walemavu Tanzania(CHAWATA)Mkoa wa Mwanza Nicolous Bwire ameishukuru VSO kwanza kwa kutambua uwepo wa kundi la watu wenye ulemavu kwani zimekuwelo taasisi na mashirika mengi nchini hapana hayakuweza kukumbuka kundi hilo.
Hata hivyo Ofisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Sitta Singibala ameeleza kuwa jambo walilofanya shirika hilo ni zuri na wameisaidia serikali kupitia Idara hiyo ya Maendeleo ya Jamii.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi