Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
Wananchi wanaopita katika standi ya mabasi ya MAGUFULI wilayani Ubungo wameanza kupimwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kwa kutumia gari la Kliniki tembezi lenye vipimo maalum .
Hayo yalisemwa na mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Manispaa ya Ubungo Dkt.Catherine Saguti November 23/2023 wakati wa Mkutano kuhusu utekelezaji wa MAF -TB yalioshirikisha washiriki kutoka Wizara ya Afya,Idara,Taasisi za Serikali na waandishi wa habari katika Mkutano huo Mkoa Dar es Salam.
“Manispaa yetu ya Ubungo tumeanza mikakati ya utekelezaji wa maagizo aliyotoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwajibikaji wa kisekta wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu (MAF -TB)”alisema Saguti.
Mratibu Uraghibishi na Mawasiliano Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma, Julius Mtemahanji, alisema malengo ya Serikali ni kutokomeza kifua kikuu na kuwa na wagonjwa chini ya 10 kati ya watu 100,000.
Mwenyekiti wa Tanzania Stop TB, Dk. Peter Bujari,Mratibu wa Uraghibishi na Mawasiliano Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma, akizungumza wakati wa mkutano kuhusu Mpango wa uwajibikaji wa kisekta wa mapambano dhidi ya kifua kikuu (MAF – TB).
Takwimu za Serikali za mwaka 2022 zinaonyesha kwa sasa kuna wagonjwa wapya 128,000 sawa na asilimia 64 ya wagonjwa wote waliotarajiwa kugundulika kutokana na makisio ya WHO lakini asilimia 36 bado hawajatambulika.
“Kila mgonjwa mmoja ana thamani kubwa kwa sababu tusipompata anaendelea kuambukiza wengine,” alisema Mtemahanji.
Aidha alisema kwa mwaka 2021 vifo kutokana na ugonjwa huo vilikuwa 26,800 sawa na vifo 71 kwa siku .
Mpango huo ulibuniwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2018 kwa ajili ya kuratibu ushiriki wa sekta na wadau katika kutokomeza kifua kikuu ifikapo 2030.
Miongoni mwa taasisi hizo ni Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi ambapo Mratibu wa Mawasiliano wa mpango huo, Isabela Chilumba, alisema wameanza kujenga uwezo katika ngazi zote za wizara hiyo kuhusiana na mpango huo.
Chilumba alisema; “Tumeanzisha mpango kazi mdogo ili kujenga uwezo katika ngazi zote za Wizara ya Ardhi kulingana na muundo mpya wa wizara…changamoto kubwa ni uelewa katika jamii.
Naye Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Seif Mbarouk, alisema wameanza kuwaashirikisha wadau mbalimbali na kupanga mikakati maalumu ya kutokomeza ugonjwa huo.
“Tutakutana na sekta nyingine kama ya usafirishaji kwa sababu kumekuwa na changamoto ya msongamano wa watu katika vyombo vya usafiri zikiwemo daladala, mabasi ya mwendokasi na treni, tukikaa nao pamoja tutaweza kuweka mikakati maalumu ya kupambana na kifua kikuu ili kufikia malengo ya kukitokomeza ifikapo mwaka 2030,” alisema
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa