Na Penina Malundo Timesmajira Online
KUNDI la Wanawake Walemavu kutoka Jumuiya ya Wanawake ya Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (Shivyawata) na Taasisi ya Sauti ya wanawake Walemavu limekabidhia simu 30 ili kuwasaidia kwenye mawasiliano.
Mkuu wa Kitengo na Ufuatiliaji na Uthamini wa Shirika Kimataifa linalofanya watu wenye ulemavu la Add International, Shabani Abeid amesema, taasisi yao imeona ni jambo jema la kuwasaidia watu wa kundi hilo katika kuwarahisishia mawasiliano.
Amesema, simu hizo ni vifaa saidizi katika kuwarahisishia wanawake kuwasiliana kwenye mambo mbalimbali na kupata taarifa zinazoendelea ndani ya nchi.
Abeid amesema, Shirika lao lilifanya tafiti mwaka 2017 zilizohusisha kujifunza changamoto wanazopitia wanawake na wasichana wenye ulemavu hasa katika ukatili hapa nchini.
“Kutokana na ugonjwa uliokuwepo awali wa Corona tuliamua kuja na hizi simu ili kurahisisha katika mawasiliano hata kama wakiwa na vikao kuwasiliana moja kwa moja bila kuwa na muingiliano,”.
“Pia tunaamini kupitia mradi huu tutawafikia walemavu wengi zaidi kwani unatarajia kuisha mwaka 2022 tutaendelea kusaidia jamii ili kuwarahisishia kupata taarifa mbali mbali,”Amesema
Mwenyekiti wa wanawake na watoto wenye ulemavu Tanzania, Nuru Awadhi amelishukuru Shirika la Kimataifa la Add kwa Msaada waliowapatia utajkaoweza kuwasaidia katika mawasiliano.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja