Na Sophia Fundi, Timesmajira Online,Karatu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha Juma Hokororo amewataka wenyeviti wa vitongoji kushirikiana na wataalam katika kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao ikiwemo zuala la ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza na Wenyeviti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Karatu katika kikao chao amesema kuwa serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Karatu hivyo wenyeviti watoe ushirikiano katika kutekeleza miradi iliyoko katika maeneo yao.
“Naomba tushirikiane katika kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yenu,nyie ndo wasimamizi wa miradi ambayo serikali imetolea fedha pia katika makusanyo ya ushuru tushirikiane na wataalam,,”amesema Hokororo.
Amesema Kuwa halmashauri hiyo imepata mafanikio makubwa katika ukusanyaji wa mapato ambapo katika robo ya mwaka wamekwisha kusanya asilimia 45 ambayo ilitakiwa ikusanywe hadi Desemba.
“Tuongeze juhudi katika ukusanyaji wa mapato ili tuweze kutekeleza miradi ya wananchi na kufikia malengo tuliyojiwekea,”amesema Hokororo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Karatu Yuda Morata amempongeza Mkurugenzi kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizoko ndani ya mamlaka hiyo ikiwemo suala la mishahara ya walinzi na posho za Wenyeviti.
“Tulikuwa na changamoto ya mishahara ya walinzi ambayo tulihangaika nayo muda mrefu lakini ulivyokuja hakuna tena changamoto hiyo na walinzi wetu wanalipwa kwa muda unaotakiwa tunakupongeza sana,”amesema Morata.
More Stories
Bei za mafuta Novemba 2024,zaendelea Kushuka
TARURA yaomba Mkandarasi aitwe
Ilemela yakusanya bilioni 3.7.robo ya kwanza