- Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo.
Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.
Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko Hilo.
Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.





More Stories
TAMWA yakumbusha jamii kupinga ukatili wa kijinsia kuelekea siku ta wanawake Duniani
Wanawake washauriwa kuchangamkia fursa za uchumi
Aida:Wanawake wakipata haki zote itapunguza migogoro