November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chunya yatoa chanjo ya polio kwa watoto kwa asilimia 160

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Chunya

UTAYARI wa wananchi katika zoezi la utoaji wa chanjo ya Polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya umefanikisha Wilaya hiyo kutoa chanjo hiyo kwa asilimia 160.

Zoezi la chanjo ya polia kitaifa limefanyika kuanzia Septemba 21-24,2023 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ililenga kuchanja watoto 56,979 lakini imefanikiwa kuchanja watoto 91,501 ambao ni sawa na asilimia 160 na kuvuka lengo kwa zaidi ya asilimia 60 huku wilaya inayofuatia ikiwa na asilimia 132.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Chunya , Blasio Kabwebwe amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutokana na maandalizi sahihi yaliyofanyika kabla ya zoezi kuanza, ushirikiano wa viongozi wote katika halmashauri hiyo bidii na kujituma kwa wataalamu walioshiriki katika pamoja na utayari wa wananchi baada ya kupewa elimu juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Akizungumzia mafanikio ya zoezi hilo ,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chunya Dkt.Darson Andrew amesema Chunya inafanya vizuri sio kwenye chanjo ya Polio awamu hii tu bali pia chanjo zote na utekelezaji wa afua mbalimbali ikiwemo za lishe ambapo kwa awamu hii Chunya ilishika nafasi ya tatu kitaifa.

Halmashauri hiyo iliongoza kimkoa na ameongeza kuwa kwa namna ambavyo viongozi wanavyowapatia ushirikiano basi Chunya itaendelea kufanya vizuri.

Wataalamu walioshiriki kuhakikisha zoezi linafanikiwa namna ambavyo waratibu na viongozi kwa ujumla walivyowapatia ushirikiano katika kutatua changamoto kabla ya zoezi, wakati wa zoezi na hatua za mwisho za kukamilisho kazi hizo jambo ambalo wametaja kuwaongezea morali ya kufanya kazi kwa bidii na weledi na hatimaye kuvuka lengo lililokusudiwa