Na Mwandishi wetu, Timesmajira
SHIRIKA la WaterAid Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang ,
wamezindua utekelezaji wa miradi miwili ya maji na usafi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.
Mradi huo unawanufaisha takribani wananchi wa Hanang wasiopungua 11,436 wanatarajiwa kufikiwa na miradi hiyo.
Akizungumza hivi karibuni mkoani Manyara katika Wilaya ya Hanang wakati wa hafla ya ukabidhiwaji wa miradi hiyo,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la WaterAid Tanzania,Gloria Kafuria amesema tangu mwaka 1998 waliingia katika Mkoa huo katika kuwahudumia wananchi wa wilaya mbalimbali na mpaka sasa wameweza kukamilisha zaidi ya miradi 22.
Amesema miradi hiyo ina lengo la kufikia kila mtanzania aishie katika wilaya ya Hanang kwa kupitia elimu
,uhamasishaji ,tafiti na uwezeshaji chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Serikali ya Uingereza
(FCDO) kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kafulila amesema mradi wa kwanza unalenga kuboresha huduma za maji, vyoo bora na usafi binafsi katika vituo vya kutolea huduma za afya viwili na shule moja vilivyopo katika vijiji vya Gawidu na Gidamula
wilayani hapo Hanang.
“Mradi huu upo chini ya ufadhili wa shirika la kidini liitwalo The Church of Jesus Christ of Latter -day Saints na utatekelezwa ndani ya mwaka mmoja,”amesema na kuongeza
“Mradi wa pili umelenga kufanya utafiti wa mabadiliko ya tabia na ushirikishwaji wa jamii kwa
ajili ya ulinzi wa vyanzo vya maji kwa huduma endelevu za maji safi na salama kwa wanachi,”amesema.
Amesema mwezi Juni mwaka huu, shirika la WaterAid Tanzania liliadhimisha miaka 40 ya utendaji kazi
wa taasisi ya WaterAid nchini Tanzania ambapo dhima ya shirika ni kuona utu wa binadamu
unakamilika na anahitaji kuwa na maji safi na salama, choo bora pamoja na siha binafsi.
“Tunaamini upatikanaji wa mambo haya matatu utamwuepusha mtanzania na magonjwa yatokanayo na uhaba wa maji pamoja na uchafu,”amesema na kuongeza
” Matarajio yangu kwamba
kupitia mawasilisho ya kina ya miradi yote miwili kutoka kwa wataalamu wa WaterAid na Halmashauri
pamoja na mawasilisho ya taarifa za hali halisi, usanifu na mipango kazi ya miradi tutaweza
kutengeneza mikakati na mbinu sahihi za utekelezaji wenye tija na mafanikio kamili,”alisisitiza.
Awali akiongea katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang,Janeth Mayanja amewashuruku
shirika la WaterAid Tanzania kwa kuwapelekea neema ya miradi hiyo katika wilaya ya Hanang pamoja na
wafadhili wa miradi hiyo FCDO pamoja na The Church of Jesus Christ of Latter -day Saints.
More Stories
Mwanasheria Mkuu apiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa
CHADEMA yasikitishwa mawakala wao kuzuiliwa
Rais Samia amlilia Dkt. Ndugulile