Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Airpay Tanzania imetambuliwa na kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoa huduma za uhakika za malipo ya fedha kwa njia ya kidigitali,katika kuhakikisha watanzania waliopot wanapata huduma hiyo.
Akizungumza Jana Visiwani zanzibar, Mwanzilishi wa Kampuni hiyo Kunal Jhunjhunwala amesema wanafuraha kupokea leseni hiyo ya huduma za malipo kutoka BOT,inaashiria kujitolea kwao katika kupanua huduma za kifedha kidijitali barani Afrika.
Amesema mafanikio hayo yanaashiria hatua kubwa kwa Kampuni yao ya Airpay Payment Services Private ambayo ilianza safari yake Februari 2023 na kupatiwa fursa ya kuendesha huduma hiyo nchini.
“Kampuni yetu itahakikisha inatekeleza shughuli zake kwa ufanisi na kulinda kila taarifa ya mtumiaji wake,
Airpay iliishirikisha Kampuni ya Ushauri ya Twigalpha yenye makao yake makuu nchini Tanzania kwa lengo la kutoa mwongozo wa kimkakati wa upanuzi wake barani Afrika,”alisema na kuongeza
“Ushirikiano huu ulileta majadiliano na warsha ya wiki nzima juu ya jinsi gani Airpay itakavyotoa mwongozo wa njia kuelekea Zanzibar ya Kidigitali Kwanza na zaidi ya uzuri wa Tanzania wa asili na vivutio vya kuvutia vya utalii, kuna fursa ya kweli kwa Airpay kuchukua sehemu muhimu katika safari ya kidijitali nchini ya kujenga jamii na uchumi usiotegemea mzunguko wa pesa taslimu,”amesema.
Kwa upande wake Mwanzilishi Mwenza wa Airpay Tanzania, Yasmin Chali alisema kampuni hiyo bado imejitolea kutoa suluhu za malipo za kiubunifu kwa usalama na zinazoweza kufikiwa kwa biashara na watumiaji barani Afrika.
“Nyuma ya teknolojia ni mwananchi ambaye anahitaji kuwa na uwezo wa kuamini huduma za kifedha za kidigitali ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku, sio kutuma na kupokea pesa tu. Tulikubali kufanya kazi na Airpay kwa sababu miongoni mwa watu wengi wanaotakia mema nchi, sisi kama waongozaji wa teknolojia ya Kiafrika na wafuatiliaji wa kufuatilia, tuliona imani na uaminifu ambao shirika hili lilikuwa nao.
Chali ameaema leseni hiyo ya huduma za malipo iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania inasisitiza kujitolea kwa kampuni hiyo kufuata mahitaji ya udhibiti wakati wa kutoa huduma za malipo ya kisasa.
Naye Makamu Rais na Meneja Mikakati wa Kampuni hiyo, Mihayo Wilmore amesema leseni hiyo mpya inaipa kampuni uwezo wa kufanya kazi ndani ya mfumo ikolojia wa fedha wa Tanzania, na hivyo kuimarisha uwepo wake barani Afrika.
“Safari hii haikuanza Februari, imekuwa na mchakato wa subira na machungu kwa miaka 30 iliyopita. Hakika tulikatishwa tamaa na hata kutaka kutupa taulo na kutoka nje ya ulingo. Airpay inaleta msisimko na hari mpya katika mfumo wa ikolojia wa kidijitali nchini Tanzania,”amesema na kuongeza
“Kampuni itashirikiana kwa karibu na mamlaka ya Tanzania, wabia na wadau ili kuhakikisha matumizi ya uhakika na salama kwa watumiaji wote wa jukwaa la huduma zake za malipo,” amesema
Aidha amesema kuwa Airpay ni kampuni ya kwanza ya kutoa huduma za fedha ya India iliyojumuisha huduma za kifedha za aina mbalimbali inayowawezesha watumiaji, wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo katika mkondo wa mwisho wa huduma, na hivyo kupelekea ujumuishaji wa kweli wa kifedha.
Kampuni hiyo inaushirikiano na zaidi ya taasisi za kifedha 200,huku washirika wa kifedha zaidi ya 1000. Kimataifa Airpay inamtazamo wa kutanua nyayo zake katika Afrika na Mashariki ya Kati
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa