Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
KIJANA mmoja mkazi wa Ilemi jijini Mbeya anayeitwa Humphrey Kihali (25)anayedaiwa kuwa ni mgonjwa wa akili anatuhumiwa kumuua baba yake mzazi kwa kumpiga na ubao kichwani .
Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anthony Mkwawa amesema kuwa kufuatia tukio hilo jeshi hilo linamshikilia kijana huyo .
Ambapo Kaimu Kamanda Mkwawa amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 10 mwaka huu majira ya saa 10.45 jioni huko Ilemi baada ya mtuhumiwa huyo kumvizia baba yake mzazi anayeitwa Francis Kihali akiwa chumbani kwake na kisha kumpiga na ubao kichwani.
Baada ya tukio hilo alikimbizwa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa ajili ya matibabu ambapo alifariki dunia Septemba 11 mwaka huu majira ya saa 1.30 asubuhi akiwa anaendelea kupatiwa matibabu..
Hata hivyo Mkwawa amesema kuwa uchunguzi wa awali ulibainisha kuwa mtuhumiwa huyo ana tatizo la akili na uchunguzi ukikamilika hatua zingine za kisheria zitachukuliwa.
Hata hivyo Kaimu Kamanda huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi ambao wana changamoto ya watoto wenye matatizo ya afya ya akili kuchukua tahadhari kwa kuweka uangalizi madhubuti na kufuata maelekezo ya utumiaji wa dawa wanazopewa ili kuzuia madhara makubwa kama haya yasitokee.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â