Na Mary Margwe, Timesmajira Online, Ruangwa
Meneja wa kampuni ya Elianje Genesis Limited Philbert Simon Massawe ameiomba serikali kuongeza nguvu katika suala la kukatika mara kwa mara kwa umeme kwenye mgodi huo.
Ameeleza kuwa kitendo hicho kinawaladhimu kuingia gharama kubwa ya kupata nyenzo mbadala ya umeme kama nishati ya diseli na petroli wakati mwingine huwa hazipatikani kwenye vituo vinavyouza mafuta hayo.
Massage ameyabainisha hayo hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea na kujionea namna ambavyo mgodi huo unaendesha shughuli zake.
Massawe amesema ni vema serikali ikaendelea kuwashika mkono katika kukabiliana na changamoto hiyo ili waweze kukabiliana na oda mpya walizopata kwenye maonesho ya madini na fursa za uwekezaji yaliyofanyika katika viwanja vya soko jipya Kilimahewa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
” Licha ya kuwa bado kuna mapungufu machache lakini hatuwezi kuilaumu serikali moja kwa moja awali hatukua na nguvu kubwa ya umeme ulikuwa unakatika karibia siku 5-7 kwa wiki, lakini kwa sasa Serikali imepigwa hatua kubwa japo kuna mapungufu machache, niiombe kuongeza nguvu kwa upande wa nishati,”amesema Massawe.
Massawe amesema serikali imewatoa kwenye kiwango kidogo cha chini lakini kwa sasa ihakikishe inawavusha na kuwawezesha kufikia kwenye uchimbaji mkubwa ili lile neno halisi la mapinduzi ya madini liweze kutimia.
Akiongelea suala la kukabiliana na ajira,, Massawe amesema kampuni hiyo imefanikiwa kuajiri zaidi ya wafanyakazi 200 wengi wao wakiwa ni vijana kutoka Mtwara na Lindi.
” Tunaelewa umuhimu wa kuwekeza katika jamii yaani rasilimali watu ndio maana tumewajengea uwezo wafanyakazi wetu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na katika mazingira ya usalama mkubwa,”.
Amesema kampumi ya Elianje Genesis inayostawi kwa kasi imedhihirisha dhamira yake thabiti katika uchimbaji wa Madini mbalimbali hapa nchini ikiwemo Madini ya Graphite, Nikei, Chuma, Green Garnet, Dhahabu, na Copper.
Akielezea baadhi ya mafanikio yaliyofanywa na kampuni hiyo kwa jamii imeweza kusaidia katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuunganisha miundombinu ya barabarani za vijiji na vijiji, kujenga madarasa katika shule zinazozunguka mgodi pamoja na kuchimba kisima cha maji kwa jamii.
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â