Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu.
Katika mabadiliko hayo, Mhe. Rais ameanzisha nafasi ya Naibu Waziri Mkuu na kuifuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake kuunda wizara mpya mbili ambazo ni: Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.
Aidha, ameimarisha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuongeza nafasi ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu watakaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki.
Katika mabadiliko hayo, Mhe. Rais amemteua Naibu Waziri Mkuu, Mawaziri wanne (4), Naibu Mawaziri watano (5), Makatibu Wakuu watatu (3) na Naibu Makatibu Wakuu watatu (3). Vilevile, amewabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu. Mabadiliko hayo ni kama ifutavyo:
More Stories
Waliombaka, kulawiti binti wa Yombo, Dar jela maisha
BREAKING NEWS: Rais Dkt Samia afanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali usiku huu
Rais Dkt.Samia aridhia ombi la Kinana kujiuzulu