Na Ashura Jumapili, Timesmajira Online, Bukoba
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu Abdalla Kaim, amewataka wataalam wenye dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kuhakikisha inatekelezwa kwa kiwango bora kama Serikali ilivyo kusudia.
Kaim ,ametoa kauli hiyo leo wakati wa Mwenge wa Uhuru ulipozindua vyumba 12 vya madarasa katika shule ya sekondari Kashai iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Hiyo ni baada ya kubaini mapungufu madogo katika samani za darasani ambazo ni meza na viti nakuwataka kufanya marekebisho huku akisisitiza wataalamu hao waliopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maendeleo kuwa makini ili kuhakikisha inatekelezwa katika kiwango kinachotakiwa na kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa.
“Mwenge wa Uhuru umefika shuleni kukagua na kupokea taarifa kuhusu mradi, umefanya ukaguzi wa nyaraka mbalimbali sanjari na kujionea ubora na viwango vilivyozingatiwa , Baada ya kukagua nyaraka tumejiridhisha zipo sawa,”amesema Kaim.
Hata hivyo amesisitiza juu ya uwepo wa nyaraka za miradi maeneo husika yanayotembelewa nakukaguliwa na Mwenge wa Uhuru kwaajili ya kujiridhisha na kuondoa usumbufu.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi