Na Esther Macha, Timesmajira , Online, Mbeya
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt,Angelina Mabula ameagiza watendaji wa wizara hiyo kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi hususani vijijini kuhusu umuhimu wa kupata hati za kimila za kumiliki ardhi.
Dkt,Mabula amesema hayo mara baada ya kutembelea banda la Wizara hiyo katika maonesho ya wakulima Nane Nane ambayo kitaifa yanafanyika jijini Mbeya.
Amesema kuwa uelewa mdogo wa wananchi hususani kwa Mkoa wa Mbeya kumechangia mwamko mdogo wa kurasimisha ardhi na kupata hati ambapo kati ya watu 100,000 watu 28,000 pekee sawa na asilimia 26 wana hati miliki.
“Kiwango hiki ni kidogo sana kwa Jiji kama la Mbeya nataka watendaji wote wa Wizara yangu kuhakikisha mnawafikia wananchi na kuwapatia elimu ya umuhimu wa hati miliki za kimila ili kuweza kuendeleza maeneo yao sambamba na maeneo ya kilimo na ufugaji,”amesema Dkt.Angeline.
Amefafanua kuwa wananchi wanaweza kukosa haki zao wakati ardhi ni yao wakashindwa kuendeleza kwa sababu ya kukosa hati miliki kuna watu wanashindwa kuendeleza mwisho wa siku inaibuka migogoro ya mipaka.
Aidha katika hatua nyingine amesema kuna kila sababu ya watendaji wa idara ya ardhi kuwafuatilia wananchi ambao hati zao zimetoka lakini wanashindwa kuzifuata katika idara husika hali inayo sababisha kukaa muda mrefu kwenye masijala za serikali.
“Niwatake watanzania wenzangu ambao mliomba hati miliki za kimila na kushindwa kuzifuata licha ya jitihada za kuwatafuta kutofanikisha kujitokeza kuzichukua,”amesema Dkt.Angeline.
Pia amesema kuwa Serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kukusanya kodi za ardhi kwa makato kwenye mfumo wa ununuzi wa nishati ya umeme ili kuwapunguzia wananchi malimbikizo ya madeni.
“Mfumo huu utawasaidia wananchi kuondokana na mrundikano wa tozo za kodi ya ardhi sambamba na kupokea taarifa za madeni ya kodi kwa mfumo wa simu za kiganjani,”amesema.
Mmoja wa wananchi waliotembelea banda hilo la Wizara ya Ardhi Hamid Juma amesema uwepo wa wizara hiyo ya kwenye maonesho hayo ni fursa kwa wananchi kujifunza vitu mbalimbali vinavyohusu ardhi katika maeneo mbalimbali hususani maeneo ya vijijini.
“Hii fursa kubwa sana kwetu kwani wengi wetu hata hizi hati kimila huwa hatufahamu taratibu zake kwa undani sana kupitia maonesho haya tumejifunza vitu vingi ambavyo kuanzia sasa vitakuwa msaada mkubwa sana,”amesema.
More Stories
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta