Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Vijana wenye ulemavu 48 ni miongoni mwa wanaufaika 400, wa mradi wa kuimarisha ujasiriamali na ajira kwa vijana(EYEE),ambao kupitia mradi huo wameonesha ni kwa namna gani kundi hilo lina uwezo wa kufanya shughuli za kujiingizia kipato na kuondokana na dhana hasi ya kuwa tegemezi katika jamii.
Mradi huo wa awamu ya pili unafadhiliwa na Taasisi ya Standard Chartered Foundation unaotekelezwa na shirika la Voluntary Service Overseas (VSO) kwa kushirikiana na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) na Serikali ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na Wilaya ya Sengerema.
Ambao lengo la mradi huo ni kuwawezesha vijana wa kike na kiume wakiwemo walemavu kushiriki katika shughuli za ujasiriamali kuanzia hatua za awali za uanzishaji wa biashara ili waweze kukua katika biashara kwa kuongeza kipato na wigo wa masoko.
Akizungumza na Timesmajira Online katika banda la VSO kwenye maonesho ya wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi kwa niaba ya Kaka yake Emmanuel Balizuka ambaye ni mlemavu wa macho na mnufaika wa mradi huo,Agnes Balizukaa amesema kuwa kupitia mradi huo unawasidia kusomesha watoto na mahitaji mbalimbali ambapo hata kaka yake ambaye ni mlemavu wa macho haendi kuomba omba mtaani hivyo ananufaika kupitia mradi huo wa kuimarisha ujasiriamali na ajira kwa vijana kwa kutotolesha vifaranga na kuuza kuku wake.
“Mimi nilikuwa sijui namna ya kufuga vizuri kuanzia kuku akiwa na siku moja hadi wiki mbili namna ya kuwalisha vizuri pamoja na chanjo lakini VSO wametuleta hapa na nimepata elimu ambayo itanisaidia pia na imewezesha wengine mashine ya kutotoleshea kuku akiwemo kaka yangu Emmanuel kwa ajili ya kutotolesha vifaranga na kuuza kuku kisha kujipatia kipato ambacho kinamsaidia yeye kupata mahitaji na hata nyumbani anatusaidia pia,”.
Anthony Yohana mmoja wa wanufaika wa mradi huo ambaye ana ulemavu wa macho(uoni hafifu), ameeleza kuwa baada ya kusaidiwa na VSO biashara yake ya kuuza kuku na mayai imeimarika kwani sasa anauza hadi vifaranga vya kuku baada ya kupewa mashine ya kutotoleshea vifaranga na shirika hilo kupitia mradi huo.
“Biashara imekuwa na kuimarika tofauti na kipindi cha nyuma kabla sija shikwa mkono na VSO kwani nilikuwa nafanya biashara lakini sikuwa na mpango kazi wowote kutokana na kutokuwa na ufahamu huo lakini kwa sasa nafanya mambo yangu kwa mpango,”amesema Yohana.
Hata hivyo ametoa wito kwa vijana wenye ulemavu kuacha dhana hasi ya kuwa hawawezi bali wafanye biashara kwani ndio njia pekee ya kuwatoa katika maisha yao na wanapo anzisha shughuli za kujiingizia kipato watapata watu wa kuwashika mkono kama yeye alivyoshikwa mkono na VSO.
“Nilianza kufanya biashara mwenyewe sikuwa na mtu wa kunisaidia wala wakunishauri hivyo unaweza kuanzisha mradi na watu wengine wa kakuona tunatakiwa kuwa majasiri siyo kusema kuwa mimi nina ulemavu siwezi kufanya kitu hapana kama akili ipo vizuri haina madhaifu yoyote unaweza kufanya vitu vyako ambapo kuanzisha kitu ni akili tu siyo ulemavu wa macho na mengine ni kawaida tu kama watu wengine,”amesema Yohana.
Pia amesema shirika mbali na kumpatia mashine hiyo limempatia elimu mbalimbali ikiwemo masuala ya fedha kwa kuweka akiba,namna ya kutafuta masoko ambayo imemsaidia kupata masoko pia kutunza akiba ambapo mwanzoni alikuwa ana mpango huo na sasa ameanza kuweka akiba na kutunza kumbukumbu za biashara yake.
“Ninahitaji sana kuendeleza mambo hayo ili VSO waweze kusaidia wengine na mashine hii ya kutotolesha naitumia mwenyewe kutokana na mafunzo niliopatiwa na shirika kwani hata nyumbani naishi na mke wangu ambaye na yeye ana ulemavu kama wangu kwenye matumizi hainipi shida hivyo vijana wenye ulemavu wasijione hawawezi,”.
Kwa upande wake Mshauri wa shughuli za vijana mradi wa EYEE VSO Mwanza Ezboni Mnahi, amesema kupitia mradi huo wa awamu ya pili jumla ya wanufaika ni 400 kati yao 48 sawa na zaidi ya asilimia 10 ni vijana wenye wenye ulemavu ambao wa kike ni 28 na kiume 20, unatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2022 hadi 2023.
“Katika mradi wetu tumefanikiwa kufikia asilimia 10 ya vijana wenye ulemavu ambao kimsingi ni vijana ambao wamekuwa wakisahaulika na jamii imekuwa na mtazamo hasi juu yao kuwa hawawezi kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na biashara kwaio tumekuwa tukiwajengea uwezo hao na vijana wa kawaida na kuwashauri namna ya kuendeleza biashara zao na elimu ya fedha,”amesema Ezboni na kuongeza kuwa
“Tumefanikiwa kuhakikisha vijana wetu wenye ulemavu wanapata fursa nje kupitia sekta binafsi na kuweza kupata masoko ya kuuza bidhaa zao tunajivunia kuona vijana Hawa ambao jamii imekuwa na mtazamo hasi juu yao kimsingi kupitia mradi wetu huu wamefanikiwa,”.
Naye Ofisa Uendelezaji Biashara wa SIDO Mkoa wa Mwanza Maneno Maporo,amesema kuwa wadau ambao wamekuwa wakifanya nao kazi ni VSO katika kuhakikisha wanasaidia wajasiriamali ikiwemo wenye ulemavu kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ya kutengeneza vitu na kuweza kujiajiri pamoja na mafunzo ya kukuza biashara.
“Baada ya mafunzo hayo tumekuwa tukiwasaidia kuwapeleka katika taasisi nyingine ikiwemo Brela ilimkusajili biashara ,TRA kupata tini namba,leseni ya biashara na tumeenda mbali zaidi tunawaunganisha na TBS ili wakalime bidhaa kama hazina madhara kwa mtumiaji wa mwisho na tumewasidi na wameweza kufanya vizuri,”.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa