November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nduhiye awataka watumishi kutunza siri

Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online

Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wametakiwa kuzingatia miiko na utunzaji siri za Serikali pamoja na kuongeza ari ya utendaji kazi na utekelezaji wa majukumu ya Bodi hiyo ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye, akihutubia Menejimenti na Wafanyakazi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (hawako pichani), kwenye kikao cha faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.

Akizungumza katika kikao cha Wajumbe wa Menejimenti na Watumishi wa Bodi ambacho kimefanyika mkoani Singida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye, amesema utoaji siri za Serikali ni jambo la hatari ambalo linaweza kuleta madhara na taharuki kwa jamii.

Kaimu Meneja Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, akisoma taarifa yake kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa kikao cha faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.

Akizungumzia kikao hicho ameeleza kuwa kitasaidia kubadilishana uzoefu, kujenga mshikamano na kuchochea morali ya ufanyaji kazi kwa watumishi hivyo kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa bodi hiyo.

Hata hivyo dhi ya viongozi na watumishi ambao wamehudhuria kikao hicho wameeleza umuhimu wa utunzaji siri na madhara ya kutofanya hivyo.

Baadhi ya Watumishi wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Ludovick Nduhiye hayupo pichani wakati akifungua Kikao cha Faragha cha Bodi hiyo kinachofanyika kwa siku mbili mkoani Singida.

Sanjari na hayo wamewapongeza viongozi wa bodi hiyo kwa kuona haja ya kuwa na kikao kicho ambacho wanaamini kitakuwa mwarobaini wa kuondoa dosari zinazoweza kujitokeza katika utendaji kazi wa kila siku.