Na Mary Margwe,Timesmajira Online,Simanjiro
Waziri wa Madini Dkt.Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Franone Mining Kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia udongo wenye mabaki ya
Waziri Biteko alibainisha hayo juzi alipokua akizungumza na makundi hayo kwenye Mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na Mwekezaji mzawa na Mtanzania Onesmo Anderson Mbise.
Dkt.Biteko amesema huo ni utaratibu mzuri unaowafanya makundi hayo 4 kuweza kufika hapo na kujitafutia kipato ili kiwawezeshe kupunguza ukali wa maisha yao.
“Franone niwapongeze utaratibu huu mliouweka mmenifurahisha sana kuwa watu waje hapa waokote wanachotaka, endeleeni kuwaletea,tumekubalinana Onesmo kadri uzalishaji utakavyoendelea kuna mawe mengine tutaanzisha mnada wa ndani ili madalali wawe wanaenda kununua mawe mazuri wauze wapate fedha kidogo kutoka mgodi wa Franone Mining,”amesema Dkt.Biteko nakuongeza kuwa
” Sasa tungempata mwekezaji mgeni haya maneno tusingeweza kumwambia,maana angetuambia sheria ya madini ni ya kwangu msinipangie, lakini kwasababu Mwekezaji tuliyempata ni mswahili mwenzetu anajua hali zetu, watu wote tunataka kupambana na njaa na umaskini anatuunga mkono,sasa lakini wanatokea watu na vineno vineno waacheni waseme si ndio jamani ni kawaida duniani watukusema nani hapa hajawahi kusemwa si hakuna,”.
Aidha amewataka makundi hayo kutambua kuwa kazi moja tu kila mtu hapa duniani ili aende mbele anahitaji kuungwa mkono Mwekezaji Onesmo Mbise naye anahitaji kuungwa mkono ili aweze kupata moyo na kuendelea kufanya mengi makubwa na mazuri katika sekta ya madini.
Sanjari na hayo amewataka pia kutopoteza muda wao kwa ajili ya kusikiliza maneno ya watu na badala yake waendelee kuchapa kazi, Rais Samia Suluhu Hassan yupo Kwa ajili yao.
Ambapo amesema kama Rais Samia Suluhu Hassan yupo Kwa ajili ya watu wa Mirerani, nani mwingine yupo kinyume si hakuna sasa chapeni kazi achaneni na maneno yasije yakawarudisha nyuma kimaendeleo.
“Mungu awabariki, nataka niwaombee kwa Mungu kila anayekuja hapa nakutoa jasho Mungu amlipe kwa jasho lake, pata pesa kula kidogo nyingine weka tunza utahitaji pesa hutakua na nguvu ya kukimbizana nazo,leo una nguvu ya kuja hapa baada ya muda mwili huu unachoka si ndio jamani, hivyo uwe na akiba kidogo ikusaidie kesho, Mwekezaji wetu atusaidie tuwe na akiba,kile kidogo unachopata kula na wewe vizuri, soda sio mpaka uione kwenye picha ule na wewe vizuri,” ameongeza Dkt.Biteko
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja