Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limefanya msako mkali dhidi ya watu wanaojihusisha na wizi pamoja na uharibifu wa miundombinu ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) ambapo mpaka sasa limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 07.
Ambapo watuhumiwa hao wamekuwa wakiwa na vifaa mbalimbali zikiwemo nyaya za shaba, earth wire na winding za ndani ya transformer ambazo zinadaiwa kuibwa ndani ya Transformer kwenye maeneo tofauti.
Akizungumza mkoani hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa, ameeleza kuwa msako huo uliowahusisha maofisa wa Tanesco Kanda ya Ziwa ulioanza Juni 7,2023 baada ya kuripotiwa kwa taarifa za uhalibifu wa miundombinu ya serikali kwa kuiba nyaya za shaba zilizomo ndani ya Transformer pamoja na waya wa shaba unaolinda transformer (Earth wire) kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Mutafungwa ameeleza kuwa Juni 5,2023 usiku huko eneo la Sagani Wilaya ya Magu Mjini,zilipatikana taarifa kwamba kuna wahalifu wameshusha transformer hivyo Askari walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata Karoli Clement (26) mkulima na mkazi wa Kisesa akiwa na pikipiki moja yenye namba za usajili MC.819 CYU aina ya HONLG rangi nyekundu ambayo ndiyo walikuwa wakiitumia kwa usafiri baada ya wenzake kutoroka ambao wanatafutwa na Jeshi la Polisi.
Ameeleza kuwa baada ya ufatiliaji askari walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na ununuzi wa vyuma chakavu ambao pia wananunua nyaya za shaba ikiwa ni miongoni mwa vyuma chakavu.
“Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na nyaya ambazo baada ya kuchambuliwa na wataalamu wahandisi wa Tanesco,
zilionekana zinafanana na nyaya zinazotumiwa na Tanesco kwenye maeneo ya earth wire na winding za ndani ya transformer uchunguzi wa kina unaendelea ili kubaini ukweli kuhusu vifaa hivyo,”ameeleza Mutafungwa.
Kamanda huyo wa Polisi amewataja watuhumiwa waliokamatwa katika msako huo ni Daniel Magege maarufu Mwendesha(43) mkazi wa Igudija Kisesa,John Deogratias(37), mfanyabiashara na mkazi wa Nyamh’ongolo, Bahati Stanley(39) mfanyabiashara mkazi wa Igoma, Marwa Dismas( 30) mkazi wa Kangaye A,Wilson Joseph(32) mkazi wa Mecco na Ally Tarimo(52) mkazi wa Kilimahewa.
Hivyo ameeleza kuwa atuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo ametoa wito kwa wakazi wote wa Mkoa wa Mwanza kuendelea kuliamini Jeshi la Polisi na kutoa taarifa zaidi za uhalifu na wahalifu wote ili hatua za kisheria ziendelee kuchukuliwa dhidi yao na kamwe tusifiche uhalifu kwa namna yoyote ile.
“Jeshi la Polisi tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa taarifa hizo zinafanyiwa kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa,”.
More Stories
Polisi yaonya vyama vya siasa
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti