Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
WAZIRI wa Afya,Ummy Mwalimu ameipongeza klabu ya Yanga kwa kuchangia chupa 627 za damu kwa mwaka 2023 huku ikizitaka timu zingine kuiga mfano huo.
Ummy ametoa pongezi hizo jijini hapa leo Juni 14,2023 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mchangia damu duniani,ambapo amesema klabu ya Yanga imefanya jambo kubwa na la kiungwana kwa kuchangia chupa 627.
“Inginia Hersi Saidi naomba nikupongeze wewe na team nzima ya Yanga damu ni wananchi na nyinyi mliochangia kweli wananchi nawapongeza sana kwa kuchangia chupa hizi za damu,mimi ni Simba lakini kama mngeshinda kule Algeria ningehamia Yanga,
“Mheshimiwa Nyongo (Stanslaus) Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Ukimwi tunapigwa hadi kwenye damu? tunatakiwa kujipanga msimu ujao,”amesema Waziri Ummy.
Klabu hiyo iliwakilishwa na Raisi Inginia Hersi Said ambaye alipokea cheti na tuzo kwa kuchangia chupa hizo za damu.
Kwa upande wake Hersi aliwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kuchangia chupa hizo huku akidai klabu hiyo itaendelea kuchangia damu lengo likiwa ni kuokoa watanzania wenye changamoto ya damu.
“Dhamira yetu ni kuokoa maisha ya wengine na hili tutalifanya kwa nguvu zote,”amesema Raisi huyo.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025