November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waislam nchini waombwa kuwa wamoja kuepuka matabaka

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira online,Dar-es -Salaam

WAUMINI wote wa kiislam nchini bila kujali madhehebu yao wametakiwa kusimama kwa umoja kuona kwamba wote ni ndugu ili kuepuka suala la matabaka katika imani zao.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salim alipokuwa akizungumza katika Kongamano la Al-Mustafa la 28 kimataifa la Quran na Hadithi lilioandaliwa kwa ajili ya kuonesha umuhimu wa Quran katika maisha ya waislam.

Ambapo kongamano hilo limeenda sanjari na kumbukizi ya kifo cha mpenda Amani Ali Imam Khomeini ambaye pia alikuwa na tabia ya kupenda kusoma quran.

Amesema wanapomkumbuka Ali Imamu Khomeini, wao kama waislam pia wanatakiwa kukumbuka katika quran, ambapo Imam khomeni amewaelekeza waislam kuwaona wakristo kama ni jamii yao kwani kwa kufanya hivyo kutaondoa migogoro mbalimbali ndani ya jamii.

Akizungumza katika kongamano hilo Mkuu wa Jumuiya ya dhehebu la shia ithna sharia Tanzania Sheikh Hemed Jalala ameeleza kwamba ndani ya quran imam Khomeini ameusihi umma kuishi katika amani, upendo na mshikamano bila kubaguana kwa nmana yoyote hasa kupitia dini na hali za maisha ya watu

Akitoa neno la ukaribisho Mkuu wa taasisi ya Al-Mustapha ambao ndiyo waandaaji wa tamasha hilo Dkt.Ali Taqavi amefafanua kwamba moja kati ya kazi za imama khomen alifanikiwa kuondoa dhuluma ambayo ndiyo ilikuwa lengo la mitume wote.