Na Esthe Macha, Timesmajira Online,Mbeya
Askari wa wanyama pori kwa kushirikiana na wananchi wa mtaa wa Itezi Magharibi wamefanikiwa kumuua simba dume aliyeua ng’ombe wawili na punda mmoja kijiji cha llowelo Kata ya Lwanjilo Wilaya ya Mbeya.
Akizungumza na majira Juni 2,mwaka huu Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilowelo Kata ya Lwanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini, Yona Samweli amesema simba huyo aliibuka siku sita zilizopita ambapo waliotoa taarifa Maliasili ambao walifika na kuanza msako.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema tukio hilo ni la tatu kutokea katika kijiji cha Ilowelo sababu ni mapito ya wanyama kutoka Ruaha kwenda hifadhi ya Katavi.
Amesema kuwa baada ya kugundua anasakwa simba huyo aliondoka na kuvamia mtaa wa Itezi Magharibi ambapo aliuua punda watatu na ng’ombe mmoja hali iliyotishia kutoweka kwa amani kwa wananchi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Itezi Magharibi, Mario Paul amesema simba huyo alikuwa tishio kubwa ambapo wananchi hasa watoto wadogo walikosa amani ambapo walifanikiwa kumuua korongoni wakati akila mzoga wa punda.
Ofisa wanyapori Wilaya ya Chunya, Jacob Mpinga amesema baada ya askari kufanikiwa kukabiliana na simba huyo walifanikiwa kumuua na mwili wake kuchukuliwa na kuhifadhi nyara hiyo ofisi za maliasili.
Amesema hii ni kawaida kwa wanyama kutoka hifadhini wakifuata ushoroba kwenda maeneo mengine.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi