Na Esther Macha, Timesmajira, Online,Mbeya
SHIRIKA lisilo la kiserikali la wadau wa kilimo (ANSAF,) limeweka mikakati ya kuboresha kilimo cha zao la kahawa kwa wakulima ili kuongeza tija ya uzalishaji na kufikia malengo.
Akizungumza katika mkutano wa siku moja ulioshirikisha wadau , maafisa kilimo wa serikali , wafanyabiashara , sekta binafsi pamoja na wakulima kutoka mikoa mitatu ambayo ni , Mbeya, Songwe na Ruvuma,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo ,Honest Mseri amesema kwamba wamelazimika kufanya hivyo kutokana na uzalishaji kuwa mdogo.
Amesema kuwa kutokana na zao la kahawa kuwa kongwe hapa nchini ni wakati sasa wa kuboresha mifumo ya upatikanaji wa miche bora ambayo italeta tija kubwa katika uzalishaji na mikoa husika kufanya vizuri zaidi kwenye kilimo hicho.
“ Siku zote wakulima wamekuwa wakiangalia zao ambalo linawapatia kipato hivyo ili kuweza kuwavutia ni lazima kuwa na mbegu bora ambayo itakuwa msaada kwa mkulima,”amesema.
Ambapo wastani wa asilimia 90 ya kahawa inasafirishwa kwenda nje ya nchi ndio sababu kubwa ya kuwakutanisha wadau ili kutengeneza soko la ndani na kuvutia wanunuzi wengi ili kuboresha kipato cha wakulima.
Amesema kuwa lengo kubwa ni kuona zao la kahawa linaendelea kutoa fursa za ajira hususani maeneo mengi yanayolima yanakuwa na maendeleo makubwa ukilinganisha na maeneo yasiyolima kahawa ili kuongeza ushawishi wa kuzalisha kwa tija.
Kwa upande wake Meneja uzalishaji kampuni ya ukoboaji Kahawa Mbimba iliyopo mkoani Ruvuma Labeli Ulomi,amesema kuwa Mkoa wa Ruvuma una ardhi kubwa yenye rutuba ambayo inafaa kwa kilimo lakini bado haijatumika.
Ambapo Halmashauri ya Mbinga pekee ina hekta 25,000 ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya kilimo cha kahawa lakini hazijaweza kutumika kwa ajili ya kilimo hicho hivyo ni fursa kubwa kwa kilimo cha zao hilo.
Huku ikifuatiwa na Nyasa ambayo ina hekta zinazozidi 6,000 ambazo hazijatumika kwa ajili ya kilimo cha kahawa .
Meneja wa programu za utafiti wa zao la Kahawa Kanda ya Mbeya,Dismas Pangalasi,amesema kuwa jukumu lao ni kutoa mafunzo kwa wakulima pamoja na kuzalisha miche bora ya kahawa.
Kwa mwaka 2022/2023 wameweza kuwafikia wakulima 7,640 katika Mkoa wa Mbeya na Songwe kwa wilaya nne na kutoa mafunzo ya mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima 9,530.
Amesema kuwa fursa ambazo wakulima wanaweza kuzipata kutoka taasisi ya utafiti wa kahawa ambayo ipo kwenye maeneo yao ambapo wana aina 13 bora za kahawa ambazo zinazalishwa kituo cha utafiti Tacri Mbimba na mbegu hizo hazishambuliwi na wadudu.
Akizungumza na majira mmoja wa wakulima wa kilimo cha Kahawa , Jeremiah Mwaje amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akijishughulisha na kilimo cha Kahawa ambacho mwanzo alikuwa akipata kahawa kwa wingi lakini hivi sasa changamoto ipo kwenye soko na ubora wa mbegu.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi