November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Serikali yawatoa shaka wananchi kuhusu kushindwa majaribio ya treni

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

SERIKALI imewatoa shaka wananchi kuhusu muda wa kuanza majaribio ya treni ya abiria kwa kipande cha kwanza cha reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambayo imeshakamilika,nakutakiwa kuanza kujaribiwa Mei mwaka huu ambapo imesema kumesababishwa na kutokukamilika kwa wakati kwa utengenezaji wa vichwa vya treni viwili na mabehewa 30.

Hayo yamesemwa jijini hapa leo,Mei 31 ,2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wananchi kupuuza minong’ono inayoendelea kuhusu kuchelewa kwa majaribio hayo na kusema kuwa Serikali haijadanganya juu ya muda wa kuanza kwa majaribio ya treni hizo bali kilichotokea ni mabadiliko ya ratiba ya mtengenezaji yalioathiri kuja kwa vichwa hivi.

Msigwa ametaja sababu ya kutofanya majaribio hayo Mei ni kutokana na kutokukamilika kwa vichwa viwili vya treni hiyo na mabehewa 30 kutokana na changamoto katika upatikanaji wa baadhi ya vipuri vinavyotumika kwenye ukamilishaji wa vichwa vya treni ambavyo vinatoka nchini Canada ambako kutokana na changamoto ya UVIKO-19, vita na kuharibika kwa uchumi katika nchi nyingi duniani vimefanya viwanda vingi vinavyozalisha vipuri kutorudi katika ratiba za uzalishaji za kawaida.

Amesema kuwa Vipuri vilivyotarajiwa vitafungwa kwenye vichwa viwili ni miongoni mwa vipuri ambavyo vimepata madhara kutokana na changamoto hizo hivyo, mtengenezaji hakuweza kuleta kwa muda aliopangiwa.

“Tumeshindwa kuanza majaribio kwa sababu hatuwezi kuyafanya kama vichwa vya kuvuta mabehewa havijafika, Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu ukamilishaji wa vichwa hivi ili vitakapofika tuanze mara moja majaribio ya treni hiyo n kwa makubaliano mapya tuliyoingia na mtengenezaji wa vichwa vya treni, ameahidi kichwa cha kwanza kitafika mwezi Julai na kikifika tu kitaanza majaribio mwezi huo huo na Kichwa cha pili kitafuata baada ya hapo,”amesema Msigwa.

Hata hivyo amesema mabehewa, baadhi yake yameshakamilika na kati ya tarehe 2-3, Juni, 2023 yanatarajiwa kupokelewa mabehewa sita ya ghorofa kwa ajili ya kutumika kwenye SGR.

“Mabehewa hayo yamefanyiwa ukarabati na kurejeshwa katika upya wake kwa zaidi ya asilimia 85, haya ni mabehewa ambayo yametoka Ujerumani ambapo jumla yake ni 30. Mabehewa 24 yataendelea kuja kwa awamu,

“Kazi ya ukamilishaji wa mabehewa yanayoendelea kutengenezwa nchini Korea ambayo tayari mabehewa 14 mapya yalishafika na mengine 45 kazi inaendelea kukamilishwa hivyo tunatarajia mabehewa yaliyobaki yatafika nchini wakati wowote ndani ya mwaka huu na
tuna mabehewa mengine ambayo tumenunua kutoka China, tunatarajia yatafika mwakani,”amesema Msigwa.

Wakati huo huo amefafanua kuhusu taarifa ya Sekta ya Anga Tanzania kukumbwa na kashfa nzito ya ndege yake ya mizigo aina ya Boeing767-300F kusafirisha mizigo haramu kwa njia haramu ambayo haijafuata taratibu za kiforodha ambayo inasambaa kwenye baadhi ya mitandao, amesema taarifa hizo ni za upotoshaji na zipuuzwe.

Amesema Serikali inaona kwamba taarifa hizo za upotoshaji ni njia mojawapo ya kurudisha nyuma juhudi za Serikali yetu katika kukuza sekta ya anga na usafiri wa anga ambapo amesema Serikali inawafuatilia waliochapisha taarifa hiyo na hatua zitachukuliwa.

“Ndege ya mizigo aina ya Boeing767-300F bado haijafika Tanzania, haijaanza kazi rasmi, bado ipo mikononi mwa watengenezaji nchini Marekani ,Ndege hii inatarajiwa kupokelewa nchini tarehe 03 Juni, 2023,”