November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ilemela yapokea milioni 140 kukamilisha maabara,bweni

Judith Ferdinand, Timesmajira online, Mwanza

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepokea kiasi cha milioni 140 kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara za sayansi katika shule 4 za sekondari pamoja na bweni
sekondari ya Sangabuye.

Hii ikiwa ni jitihada za serikali za kuboresha mazingira na kuweka miundombinu bora ya wanafunzi kujifunza na kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na Halmashauri hiyo,ambapo imeanisha kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha milioni 120 kimepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara za sayansi huku kila shule imepokea kiasi cha milioni 30 kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara hizo.

Ambapo shule zilizopokea kiasi cha fedha hizo kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara za sayansi ni Sekondari ya Kabuhoro , Kirumba, Angeline Mabula na Kisundi.

Hatua mbalimbali za ukamilishaji zinaendelea katika shule tatu ambazo ni Kirumba,Kabuhoro na Angeline Mabula.

Aidha kiasi cha milioni 20 kimepokelewa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Sangabuye.

“Ilemela tunaendelea kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,”.