November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wahitimu wa kidato cha sita wote waitwa makambini

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT)  limewataka vijana wote waliohitimu elimu ya kidato cha sita kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria 2023.

Aidha Jeshi hilo limesema,miundombinu ya Jeshi hilo limejiandaa vyema kwa kuwa na miundombinu ya kutosha kwa ajili ya kuwapokea vijana hao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya JKT Chamwino mkoani Dodoma kuhusu wito huo wa vijana Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanapaswa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa kuanzia Juni Mosi  hadi Juni 11 mwaka huu.

“Vijana hao wamepangwa katika kambi za JKT Rwamkoma –Mara,JKT Msange –Tabora,JKT Ruvu Pwani,JKT Mpwapwa ,Makutupora JKT-Dodoma,JKT Mafinga –Iringa,JKT Mlale-Ruvuma ,JKT Mgambo na JKT Maramba –Tanga .”

Ametaja kambi nyingine kuwa ni “JKT Makuyuni-Arusha,JKT –Bulombora,JKT Kanembwa na JKT Mtabila za Kigoma,JKT Itaka Songwe,JKT Luwa na JKT Milundikwa –Rukwa,JKT Nachingwea-Lindi,JKT Kibiti –Pwani na Oljoro JKT Arusha.”

Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mabena wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT Mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

Aidha amesema,orodha kamili ya majina ,makambi waliyopangiwa na mahitaji yote yanayohitajika vinapatikana kwenye tovuti ya JKT www.jkt.go.tz.