November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NACTVET wafungua dirisha la udahili

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) wametangaza rasmi leo Mei 21,2023 kuwa wamefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wanataka kujinga na vyuo mbali mbali hapa nchini katika mwaka wa masomo 2023/2024.

Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha Jana kwenye maonesho ya vyuo vikuu yanayofanyika Katika viwanja vya stadium
Mkurugenzi wa udhibi, ufatiliaji na Tathimini NACTVET Dkt, Jofrey Oleke, amesema kwamba udahili huo wa kozi zote zinazo tolewa na vyuo mbali mbali wamefungua rasmi leo Mei 21,2023 hadi Juni 30, 2023 katika awamu ya kwanza.

“kama nilivyoaema hapo awali ni kwamba dirisha limefunguliwa Rasmi Sasa Kwa hiyo ni waombe wenye uitaji wahakikishe kuwa wanatumia fursa hiii Kwa kuanza kuomba Rasmi kwa kutuma maombi na walengwa ni wale ambao ni Wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na vyuo vyenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, nawashauri kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi wanazo zipenda”. Amesema Dkt Oleke.

“Lakini pia niwaambie kuwa Kwa wale ambao nimewataja hapo juu wawe wametimiza sifa na vigezo vya kujiunga na vyuo katika kozi walizo omba kwa mwaka wa masomo 2023/2024 na maombi hayo ya kujiunga yatumwe katika vyuo husika haraka iwezekanavyo kabla dirisha halijafungwa rasmi” alisema Dkt Oleke

Katika hatua nyingine aliwataka pia kwa wanafunzi ambao watakuwa na uitaji WA kujiunga na programu za afya pamoja na Sayansi Kwa upande wa Tanzania Bara wanapaswa nao watahitajika kuwasilisha maombi Yao pamoja na kufanya udahili Kwa pamoja kabla dirisha halijafungwa.

“Kwa wanafunzi wanaopenda kujiunga na kupitia kozi ya Afya na Sayansi Shirikishi hawa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja yaani Central Admission System _ CAS, katika tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz”. Amesema Dkt Oleke.

“Baraza pia linawashauri waombaji wote, wazazi na walezi kuhakikisha wanaomba udahili kwenye vyuo ambavyo vimeorozeshwa kwenye muongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo 2023/204 ( Admission Guidebook for 2023/204 Academic Year ) ambapo muongozo huo unapatikana katika tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz “. Aliongeza Dkt Oleke.

Aidha pia Dkt, alisema Baraza linatoa rai kwa waombaji wote kuandika taarifa zao sahihi pamoja na kutunza taarifa watakazo patiwa na Baraza bila kumpatia mtu yeyote ili kuepusha usumbufu katika zoezi zima la maombi yao ya kujiunga na vyuo katika kozi mbali mbali.