November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof. Mkenda: Serikali kuboresha mitaala ya elimu

Na Queen Lema, TimesMajira Online, Arusha

Serikali imesema kuwa inatarajia kuanza kubadiisha mtaala wa elimu hapa nchini ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye sekta ya elimu ambayo yanalenga ufanisi Kwa mtoto kuanzia ngazi ya awali mpaka ngazi ya vyuo vikuu.

Hayo yameelezwa juzi na waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akifungua maonesho ya NACT VET yanayoendelea Jijini Arusha

Mkenda alisema kuwa mfumo huo utaweza kuangalia namna ya kutoa mitaala ambayo inalenga kumfanya mtoto aweze kuwa imara kuanzia elimu ya awali

“Mtaala huo utaweza kuwa na elimu na mkondo amali ambapo pia nao utakuwa na Mafunzo machache na ambapo pia elimu jumla itaweza kwenda sanjari na Mafunzo ya vitendo hayo ndio mageuzi ambayo tunataka kuyaleta”aliongeza

Wakati huo huo aliitaka jamii sasa kuanza kulifikiria Jambo Hilo la mabadiliko ya mitaala ambayo wadau wataanza kutoa maoni Yao namna ya kuboresha zaidi mitaala mipya ambayo itaanza rasmi siku chache zijazo.

Alitoa rai kuwa kuanzia sasa wizara itaaanza kuboresha mausiano Kati ya wadau na wadau kama sekta ya viwanda na waajiri ili kuweza kupata kitu ambacho ni kizuri zaidi

Naye Bi husna Sekiboko Ambaye ni makamu mwenyekiti kamati ya Kudumu ya elimu alisema kuwa elimu ambayo sasa inaenda kufanyiwa mabadiliko itaweza kumsaidia mtoto aweze kuwa Bora zaidi hasa kwenye sekta ya ajira

Katika hatua nyingine katibu mtendaji Wa NACT VET Dkt Adolf Rutayuga alisema kuwa lengo la NACT VET mabadiliko makubwa ya kuboresha mfumo wa elimu ambayo yanaanza hivi karibuni wao kama wadau watahakikisha kuwa wanazidi kuboresha mambo mbalimbali

Dkt Adolf Alimalizia Kwa kusema kuwa watahakikisha kuwa wanazidi kuwaunganisha wadau wa vyuo sanjari na juhudi za ubunifu ili kuweza kuwajengea vijana uwezo zaidi.