November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanawake watakiwa kusimamia malezi ya watoto

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Diwani wa Kata ya Goba, Esther Ladslaus Ndoha, amewataka wazazi kusimamia mmomonyoko wa maadili kwa Vijana na Watoto wao wawalehe katika Malezi mema na kutenga muda wa kuzungumza nao .

Diwani Esther Ladslaus aliyasema hayo katika tukio la women’s day out tour ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani Wilaya ya Ubungo lililoandaliwa na Mwanzilishi wa Joyful Fondation na Jukwaa la Women’s day out .

“Nawaomba Wanawake wezangu kusimama imara katika Malezi na kuzungumza na watoto wao ili kama kuna changamoto katika Maswala ya mmomonyoko wa maadili watoto wawambie Wazazi wao alisema Esther.

Diwani Esther alisema
sasa hivi Dunia ipo katika utandawazi amewataka wazazi kuwambia watoto wao bila kificho wanapofanyiwa vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili watoe taarifa kwa wazazi wao.

Aidha aliwataka Wazazi kuwaweka watoto wao karibu na Mwenyezi Mungu Ili wawe wanakemea matendo ya ukatili .

Aliwataka Wazazi kulinda vijana na watoto wao katika kuisaidia Jamii katika Malezi Bora Ili Taifa letu liweze kupata vijana wachapa kazi wa Taifa la kesho .

Akizungumzia siku ya Wanawake iliyoandaliwa na Joyful Fondation na Jukwaa la Women’s day out alipongeza Taasisi hiyo kuwaunganisha Wanawake pamoja katika ujasiriamali na kutafuta masoko mbalimbali ya kiuchumi .

Alimpongeza Joyce Maketa Mwanzilishi wa Taasisi ya Joyful Fondation ,na jukwaa hilo la wanawake kwa kuandaa kongamano hilo wilaya ya Ubungo .

Diwani Esther aliwataka wanawake kujikwamua kiuchumi kukaza buti Ili wapambane kutoka katika hatua moja kwenda hatua nyingine .

Aidha aliwataka wanawake kubadirika wasifanye bidhaa kwa mazoea badala yake wawe wabunifu wapate masoko makubwa .

Aliwataka wanawake wa Ubungo kushirikiana na Umoja wanawake UWT katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mwanzilishi wa Joyful Foundation Joyce Maketa, alisema Jukwaa la Women’s day out lilianza January 2022 dhumuni lake kuwaunganisha wanawake kufunguka fikra, kujua fursa mbali mbali kwa kupatiwa elimu na kushiriki matendo ya kusaidia jamii kwenye makundi maalum hivyo kila wilaya inafanya kongamano la wanawake Ubungo, Ilala na kinondoni na imeshafanikiwa bado kinondoni inakuja na mwisho kuelekea kongamano kubwa la mwaka kwa jukwaa hilo linaloitwa the national women show Tz lenye kuwakusanya wanawake wote kuja kuleta bidhaa, kuonyesha na kununua katika kuweka siku maalum ya kujifunza na kununua bidhaa .

Joyce Maketa alisema Joyful Foundation na jukwaa la women’s day out imeweza kufanya ziara mbalimbali Ikiwemo kutembelea Watoto waliokatika Makao za watoto wachanga Mburahati na msimbazi center.

Alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan imeweza kufanya mambo makubwa katika kuwapa fursa Wanawake kiuchumi ikiwemo kuwapatia mikopo .