Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Fact-Cheking
Unapoelezea ‘Youtube DataViewer’ ni miongoni mwa zana ya kidijitali inayotumika kuthibitisha video ya mtandaoni kama ni ya kweli au uongo.
Zana hiyo inaweza kutumiwa na mtu yoyote ili kujiweka salama dhidi ya upotoshaji wa habari ambapo kwa sasa hali hiyo imekuwa ikikithiri kila kukicha.
Mabadiliko kasi ya teknolojia ulimwenguni yamefanya iwe rahisi kufuatilia tukio kwa njia ya video lililopo umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 kutoka ulipo kupitia simu janja. Miaka ya nyuma jambo hili halikuwa rahisi hata kidogo.
Tofauti na miaka ya nyuma ambapo vyombo vya habari pekee vilikuwa vikipeperusha habari, kwa sasa kila mtu ana uhuru wa kusambaza habari picha na video kupitia intaneti.
Uhuru huo wa kila mtu kuwa na uwezo wa kusambaza video umesababisha baadhi ya video hizo kutumika kwa nia ya kupotosha watu kwa manufaa mbalimbali ikiwemo kuongeza umaarufu au kipato.
Ongezeko la habari za uzushi kwa njia za video limesababisha wadau mbalimbali ulimwenguni kuweka jitihada za kupambana na uzushi unaotokea katika teknolojia hiyo ya picha jongefu.
Hata hivyo, si watu wote wana uwezo wa kung’amua iwapo video wanayoiona kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Facebook.
Miongoni mwa zana inayotumika kuthibitisha au kung’amua video ya uzushi ni zana ya kidigitali ya ‘Youtube DataViewer’.
Zana hiyo ni moja ya zana nyingi za kidigitali zitakazokusaidia kuthibitisha video kama ni ya ukweli au uongo.
Zana hiyo, hutumiwa kwa ajili ya kuthibitisha taarifa kuhusu video hasa muda ambao iliwekwa mtandaoni sambamba na maelezo na picha za msingi kuhusu video hiyo.
Jinsi ya kutumia
Kwa ambaye hajawahi kuitumia, katika hatua ya kwanza unatakiwa kwenda kwenye mtandao wa Google kisha tafuta neno ‘Youtube DataViewer’ kisha itakuletea unachokitafuta.
Mtandao wa Google utakuletea majibu kadhaa lakini changua ‘Youtube DataViewer’ ili uweze kutumia na kuthibitisha video husika.
Baada ya kufungua jambo la kwanza utatikwa kuweka kiunganishi (Link) cha video ambayo lazima itokane na Youtube.
Utaweza kuona jina la hiyo video, muda wa uchapishaji na sambamba na picha zote zilizotumika katika video hiyo.
Ukiachilia hizo taarifa lakini ukumbuke bado hakuna zana ya moja kwa moja ambayo mtu anaweza kuthibitisha picha jongefu isipokuwa kuchukua picha za kawaida zilizopo kwenye video husika na kuzitafutia ukweli wake.
%%%%%%%%%
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa